December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mjema kwenda kufanyakazi kwa mitazamo tofauti,ataja uelimishwaji

Na Zena Mohamed,TimesMajiraOnline,Dodoma.

Katibu wa itikadi na uenezi  wa hicho ,Sophia Mjema alisema kuwa kwa nafasi aliyopewa anaenda kufanyakazi kwa mitazamo tofauti kwani kabla ya kwenda kwa wananchi lazima idara hiyo uelimishaji uwe sawa .

Mjema ameysema hayo jijini hapa leo,Januri 24,2023,wakati akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwapokea wajumbe wa Sekretarieti mpya ya chama hicho akiwemo yeye mwenyewe.

“Lazima mabalozi wetu wakajue wananchi wanataka nini lazima ndugu zetu  tutakapokwenda kwa wananchi tutaenda mpaka ngazi za vitongoji tukajue wananchi wanataka nini,”amesema Mjema.

Amesema katika kukitangaza chama wanaccm wanatakiwa kufanyakazi  wote kwa pamoja kwani hakuna mwingine atakae kilinda chama bali ni wao.

“Nataka tukumbushane tu na wanaccm mwenyekiti wetu lazima tumtetee iwe usiku iwe mchana kazi yetu ni chama cha mapinduzi hivyo lazima tumtete Mwenyekiti wetu.

Ndugu zangu wakina baba na wakinamama, wasichana na wavulana nataka nisikie kwa mioyo yenu mkiimba chama cha mapinduzi,hivyo ndivulyo tutakavyoona maonao ya Mwenyekiti wetu atakayotuletea.

“Subiri muone mnakuja kuona chama chenu kinavyokuja kuwatetea kama kulikua na maonevu tunaenda kuyamaliza kama kuna kero tunaenda kuzimaliza ila tunakuja kwa kutoa alimu ambayo kila mtu atatambua jinsi ya kuelimishana,”amesema.

Pia amewawahakikishia wakina baba na kina mama wa chama hicho kuwa atafanya nao kazi bega kwa bega

“Kinababa nitafanya kazi na nyinyi wakinamama sitawaangusha kama mnavyojua nafasi hii toka ianze haijawahi kushikwa na kina mama hivyo sitawaangusha kwenye hii nafasi,”amesema.