Na Iddy Ally, Timesmajira Online DSM
USIMIKAJI wa mitambo ya kupima ujazo wa mafuta flow meters katika bandari ya Dar es salaam, Mtwara na Tanga utaondoa kwa kiasi kikubwa upotevu wa mafuta ikiwa ni pamoja kupata takwimu sahihi za mafuta yanayoingia nchini na kuiwezesha serikali kutoza kodi na tozo zinazostahiki zinazotokana na uingizaji wa mafuta nchini.
Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari jijini Dar es salaam Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salaam Mhandisi Yona Malaga amesema kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha uwezo wake wa kuhudumia shehena zikiwemo shehena za mafuta ya nishati, mafuta ya kupikia na gesi ya LPG.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Augusto Energy Orlando D’costa ameelezea namna mtambo huo utakavyofanya kazi kwa kisasa tofauti na awali huku Mhandisi Prof. John Bura akieleza hapo awali jinsi upotevu wa mafuta ulivyokuwa ukitoa kwa kutokuwa na mitambo mizuti ya kisasa.
Mamlaka ya Bandari Tanzania imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali na mradi huu wa usimikwaji wa mitambo ya kisasa ya kupima mafuta pindi yanaposhushwa kutoka kwenye meli utaipatia serikali mapato na tozo sahihi kwani unafanyika kwa teknolojia ya kisasa zaidi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa