January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miss Tanzania aipongeza STAMICO

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online

MLIMBWENDE Miss Tanzania 2020 Rose Manfere ametembelea Banda la STAMICO na kuipongeza kwa kazi nzuri inayofanya kwa kipindi chote cha maonesho ya 77 katika kuelimisha umma hasa kuhusu uchakataji na uongezaji thamani katika Madini, matumizi ya mkaa wa mbadala wa Rafiki Briquettes.

Akizungumzia Maonesho ya sabasaba kwa mwaka huu amesema amefurahia sana kufika katika banda bora la STAMICO na kupata elimu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na STAMICO.

Amesema ni mara chache sana elimu hii hutolewa kwa wananchi wa kawaida hivyo imekuwa na tija kubwa kwake kwa kuwa amefahamu hatua zote jinsi Madini yanavyopatikana.

Amepongeza kwa ubunifu mkubwa uliotumika kwenye muonekano wa banda na katika kutangaza bidhaa mbalimbali za Shirika na husani Mkaa mbadala na hasa jinsi utakavyosaidia kina mama wakati wa kuutumia jikoni.

Ametoa wito kwa Watanzania kutumia Maonesho haya ya Sabasaba ili wapate kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Madini na Taasisi zake.