Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Kyela.
MKURUGENZI Msaidizi anayeshughulika na Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Luteni Kanali Selestine Masalamado ameongoza ujumbe wa kutoka Nchini Tanzania kupeleka misaada ya unga, mahindi, mablanketi, mahema na madawa mbalimbali ambayo yatasaidia wahanga wa Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi.
Luteni Kanali Masalamado amesema hayo wakati Msafara wa magari ya jeshi la Wanachi wa Tanzania yakivuka mpaka wa Kasumulu wilaya ya Kyela kuelekea Mji wa Blantyre Nchini Malawi tarehe 22/03/2023.
“Natoa pole kwa ndugu zetu, wananchi wa Malawi tuko nao katika hali hii ngumu,”amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.
“Katika kuitikia hilo serikali ya Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya Majanga,”amesema
Naye Mkuu wa wilaya ya Karonga Nchini Malawi,Roderick Mateauma ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kwamba msaada huo utasaidia kupunguza athari kwa wahanga na inaonesha mahusiano ya karibu yalipo
More Stories
Madiwani Ilala watoa chakula kwa watoto yatima
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano