Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
WANAWAKE wa Kata ya Minazi Mirefu Wilaya ya Ilala, wanatarajia kunufaika na mkopo wa milioni 236,inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam kwa awamu ya kwanza.
Hayo yamesemwa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Minazi Mirefu,Mohamed Bushiri , katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa kata hiyo, Godlisten Malisa,ambalo amesema wamefanikiwa kuhakiki vikundi 17 vya awamu ya kwanza.
Aliwataka wanawake, vijana na watu Wenye Ulemavu ambao wameomba mikopo hiyo kurejesha kwa wakati ili watu wengine waweze kukopa huku wananchi wengine wanaohitaji mikopo hiyo kufika ofisi ya Mtendaji wa Kata na wamuone Ofisa Maendeleo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu, Godlisten Malisa,amewataka wananchi ambao wanapewa mikopo hiyo,wasiitumie katika vigodoro pamoja na ngoma za kutunzana,badala yake wazitumie kukuza mitaji yao.
Naye Ofisa Maendeleo Kata ya Minazi Mirefu, Jovinda Mavenda,amesema anatarajia kutoa mikopo kwa vikundi 17 awamu ya kwanza, na wale walioomba awamu ya pili watapewa hivyo amewataka wafuate taratibu na kutimiza masharti.
Sanjari na hayo Mavenda,amewataka wazazi kuzingatia kuwalea watoto wao,ikiwemo kufuatilia maendeleo ya masomo yao pamoja na wakati wa kwenda shule na kurudi nyumbani.
More Stories
Exim bank yaingia mkataba wa Zati
Rais Samia amrudisha January kwa Mama,asema kilichotokea ni kumuonya
Mipango 10 kabambe ya TPA