
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Mohamed Mtulyakwaku, amewaagiza Maafisa Elimu Kata wilayani humo kudhibiti taasisi zinazotoa mikopo ya kausha damu kwa walimu, huku akisisitiza kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya maafisa watakaobainika kuruhusu taasisi hizo kuwakopesha walimu.
Mtulyakwaku ametoa agizo hilo wakati wa kikao kazi na watumishi wa umma wilayani Nkasi, ambapo amewataka walimu kujiepusha na mikopo ya kausha damu na badala yake kukopa katika taasisi za kifedha zinazotambulika kisheria.

Aidha, amewataka watumishi wa umma kujiepusha na vitendo vya utoro kazini, akisisitiza kuwa kila ofisi, kuanzia ngazi ya kata, inapaswa kuweka mifumo ya kielektroniki ya kurekodi mahudhurio ya watumishi wanapoingia na kutoka kazini.
Ameongeza kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya watumishi watakaobainika kutohudhuria kazini bila sababu za msingi, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na nidhamu kwa utumishi wa umma.

More Stories
TMA: El Niño kuathirinmvua za Msjku 2026-2027
TANESCO kuiwezesha HWTZ kuzalisha Megawati 200 za umeme
Bombo yawatafuta waraibu 436