April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Michezo yatumika kutangaza hifadhi ya Arusha

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katika huhimiza utalii wa ndani nchini Tanzania Bwana Lomayan Komolo Simel kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa wanyama pori na utalii wameamua kutumia njia ya michezo ili kutangaza hifadhi ya Arusha iliyopo karibu na mji wa Arusha pamoja na kusapoti jitihanda za serekali ya kuzitangaza hifadhi zetu za taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari mhazilishi mkuu wa mbio hizi na mratibu mkuu mtendaji wa Arusha Park wildlife Marathon Lomayan Komolo amesema kuwa wameandaa riadha ambayo ni tofauti na kipekee Tanzania kwani Kwa asilimia mia Moja mbio zote zitakuwa ndani ya hifadhi na sio nnje ya hifadhi.

Amesema kuwa marathoni hiyo itakuwa na mbio aina tatu ambapo mbio ya kwanza itakuwa kilomita 5 Fun run, 10km na Half marathon 21km,pia mbio hizi zitakuwa zinaanza mahali moja na kumalizikia mahali moja ni one way run, yaani unamalizia huko huko bila Kirundi njuma kama mbio nyingi tulizo zoea, pia hifadhi ina mathari mazuri pamoja na wanyama ambako wakimbiaji watakuwa na fursa ya kukimbia pembezoni mwa wanyama kwahiyo watawaona wanyamapori.

Amesema marathon hiyo itakuwa na Ghaarama kidogo ambayo ndio kiingilio na marathoni hiyo usalama utakuwa mkubwa sana hivyo anawatoa watu wote hofu Kwa asilimia mia Moja usalama upo.

Amesema lengo la mbio hizo ni kutangaza hifadhi ya Arusha kwani ni hifadhi ambayo watu wengi waliopo Moshi na Arusha pamoja na mikoa jirani hawaijui lakini lengo lingine ni kuchangia fedha Kwa ajili ya kungoa magugu vamizi ambayo ni hatarishi Kwa wanyamapori ndani ya hifadhi ya Arusha.

Pia amesema kuwa marathoni hiyo pia ni fursa ya kutangaza huduma mbali mbali zinazo tolewa na wawezeshaji wa mbio hizi za Arusha Park Marathon, kukuza vipaji kwa wakimbiaji chipukizi vilevile jamii pia itajifunza mambo mengi ya uhifadhi na utalii.

Aidha amesema kuwa gharama zinatofautiana Kwa jumuiya afrika mashariki 35,000/= Kwa ajili ya kiingilio,wageni wa nje wanafanya kazi Tanzania gharama ni 120,000/= na watalii wa nje ni gharama ni 190,000Amesema kuwa Kwa wakimbiaji wote watapatiwa medali, tishert na riboni mkononi,vikombe Kwa washindi kuanzia namba 4 Hadi 10 na pesa kias kwa washidi wa 1-3 ,vile vile kutakuwa na huduma za majii, matunda na glucose ili kuwapatia nguvu wakimbiaji njiani.

Amesema kuwa Kwa wale watakojisajili Kama timu au clubs mkoani Arusha na Moshi kufikia kiwango cha watu 30 watapatiwa usafiri Bure.

Kadhalika, amesema kuwa Kwa wale ambao wana watoto wadogo watachangua gharama kidogo na pia Kwa wale watakotamani kulala vile watachangia kidogoHata hivyo katika marathon hiyo zaidi ya washiriki 400 wanatarajiwa kushiriki ambapo pia Kwa anayehitaji tiketi zipo sehemu zifuatavyoo kwa mini Arusha fika maeneo yafuatayo office ya TTB clock tower,Kipong mkabala na polisi na Jengo la Condo kaloleni ground floor chumba number 5 na Kwa mji wa Moshi unaweza kufika chuo cha wanyamapori Mweka na Kibo Cleaning services (Kwenye tawi la Viva Yanga Kilimanjaro) opposite na coffee CuringSanjari na hayo.

Mhanzilishi huyo amesema zoezi Hilo litakuwa endelevu na amewataka wanariadha kote nchini kujitokeza ipasavyo hiyo tarehe 4/12/2022 kukimbia hii mbio ya kipekee kabisa Tanzania.