Na Yusuph Mussa, TimesMajira Online, Lushoto
HALMASHAURI ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine ya kiutendaji, inajivunia kupiga hatua katika shughuli za maendeleo hususani katika sekta za elimu, afya, kilimo, mifugo na maendeleo ya jamii.
Maendeleo hayo ni matokeo ya jitihada za Serikali za kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa zimeelemewa.
Mwandishi wa makala hii amezungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Ikupa Mwasyoge, ambaye ameeleza mafanikio hayo.
ENEO LA UTAWALA
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ina eneo la Kilomita za mraba 2,300, Tarafa 5,Kata 33, vijii 125 na vitongoji 942,aidha, halmashauri ina majimbo mawili ya uchaguzi, Jimbo la Lushoto na Jimbo la Mlalo.
IDADI YA WATU
Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ina watu 350,958, kati yao wanaume ni 160,815 na wanawake 190,143.
TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA MWAKA 2021/2022 HADI 2023/2024
Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024, halmashauri imefanikiwa kukusanya na kupokea kiasi cha zaidi ya bilioni 36.8 (36,822,779,451.66) kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo mapato ya ndani ni zaidi ya bilioni 1.2(1,228,099,516) Serikali Kuu zaidi ya bilioni 20.5(20,590,657,481) na Wahisani bilioni 15.0(15,004,022,453).
MAFANIKIO KISEKTA KWA KIPINDI CHA MWAKA 2021/2022 HADI 2023/2024
Sekta ya Afya
Kwa upande wa sekta ya afya katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imefanikiwa kupokea kiasi cha zaidi ya bilioni 5.7(5,775,024,897.12) kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto.
Pia ukarabati hospitali ya Wilaya, ununuzi wa vifaa tiba,ujenzi wa vituo vya afya vinne umaliziaji wa ujenzi wa zahanati 10 na ujenzi wa nyumba nne za watumishi
MAFANIKIO
Halmashauri imefanikiwa kusajili vituo vya afya viwili na zahanati 10,kupunguza vifo vya mama na mtoto pamoja na kuondoa kero kwa wananchi ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, kwa kusogeza huduma hizo karibu na wananchi.
SEKTA YA ELIMU
Kwa upande wa sekta ya elimu katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024, halmashauri imepokea kiasi cha zaidi ya bilioni 25(25,922,553,108.65) kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule mpya nne za msingi na nne za sekondari pamoja na ujenzi wa mabweni 21.
Ujenzi wa vyumba 282 vya madarasa, umaliziaji wa maboma ya madarasa 41,ujenzi wa madarasa ya awali ya mfano 8, ujenzi wa matundu 638 ya vyoo, umaliziaji wa maabara 20, ukarabati wa shule kongwe 4.
Pia ujenzi wa mabwalo 3,ujenzi wa maktaba 4,ujenzi wa majengo 6 ya Utawala na mapokezi ya fedha za elimu bila malipo.
MAFANIKIO
Halmashauri imesajili shule za msingi 17 na za sekondari 5, ufaulu umeongezeka kwa kuwa elimu inatolewa bila malipo, kuondoa kero kwa wanafunzi ya kutembea umbali mrefu, kuondoa mrundikano wa wanafunzi darasani hivyo kuepusha uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa.
Serikali imesaidia vituo shikizi kukidhi vigezo vya kusajiliwa kuwa shule za msingi kupitia fedha za UVIKO – 19, kupunguza utoro na mdondoko wa wanafunzi, kwani wanafunzi watapata huduma bora za elimu karibu na maeneo wanayoishi, mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi.
SEKTA YA UTAWALA
Ajira mpya; Katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, halmashauri imepokea watumishi wa ajira mpya 581 katika kada mbalimbali, kupandisha madaraja, kwani katika kipindi cha miaka mitatu hiyo, Serikali imefanikiwa kuwapandisha madaraja watumishi 1,024 katika sekta mbambali na pia imefanikiwa kuwabadilishia muundo watumishi 63.
Aidha, kwa upande wa Sekta ya Utawala, halmashauri imepokea sh. 264,376,862.09 kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ya Mkurugenzi, ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara na ujenzi wa uzio wa nyumba ya Mkurugenzi na uzio wa Nyerere Square.
SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024, halmashauri imetenga na kupeleka kwenye akaunti ya mikopo sh. 362,416,654.80 kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu. Aidha, kati ya fedha hizo, kiasi kilichokopeshwa ni sh. 195,700,000 kwa vikundi 29, na kiasi cha sh. 166,716,654 kipo kwenye akaunti ya mikopo kwa kuwa zoezi la utoaji wa mikopo limesitishwa tangu Aprili, 2023.
Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 fedha zilitolewa kwa mikopo hiyo ni sh. 148,416,654, mwaka 2022/2023 ni sh. milioni 161, na mwaka 2023/2024 ni sh. milioni 53, hivyo jumla kuu kuwa sh. 362,416,654.
Aidha, halmashauri imepokea sh. 4,498,407,929. kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo TASAF sh. 3,625,862,110, shughuli za kilimo sh. 135,678,000, urasimishaji ardhi sh. milioni 208, Anwani za Makazi sh. 154,999,819, na fedha za Mfuko wa Jimbo sh. 373,868,000.
“Kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa za kuboresha miundombinu katika Sekta za Elimu na Afya.
“Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto wameshuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana na Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi kifupi cha miaka mitatu. Juhudi zote ambazo halmashauri kwa kushirikiana na Serikali Kuu inazifanya, zinalenga kuongeza vipato vya wananchi na kutoa huduma muhimu za jamii ikiwepo elimu bila malipo, afya na maji ili kupunguza umasikini miongoni mwa watu wetu” anasema Mwasyoge.
More Stories
Boost ilivyoboresha miundombinu ya elimu IlemelaÂ
Samia apongeza walimu 5,000 kupatiwa mitungi ya gesi, majiko kutoka Oryx
Uwekezaji kwenye kilimo utatimiza ndoto ya Samia ya nchi kuwa ghala la chakula Afrika