Na Jackline Martin, TimesMajira Online
KIPINDI cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kimekuwa cha mafanikio makubwa kwa upande wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADs).
Tumeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali, ambapo chini ya uongozi wake mtandao wa barabara za lami umeongezeka ukiachilia mbali zile zinazoendelea kujengwa.
Tumeshuhudia kasi ya ujenzi wa madaraja katika mikoa mbalimbali, ambayo yamesaidia kuunganisha nchi. Lakini kikubwa ambacho kimefanyika ni kuunganisha mikoa kwa mitandao ya barabara na sasa kazi hiyo inandelea kwenye wilaya.
AKizungumza na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TANROAD, Mhasidisi Mohammed Besta, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Ephatar Mlavi, alisema uongozi wa Rais Samia umekuwa na mafanikio makubwa kwa taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa Mlavi, miongoni mwa mafaniko hayo ni kutenga asilimia kumi ya bajeti ya kila mwaka ya maendeleo kwa ajili ya miradi ya mafunzo kwa vitendo.
Alidha, alisema mengine ni kutenga angalau asilimia 30 ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya upendeleo kwa wazawa.
Mengine ni kutenga angalau asilimia tano ya bajeti ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya makundi maalum.
Kuhusu ushiriki wa wa wanafunzi na wahitimu katika miradi, Mlavi, alisema kazi za matengenezo ya barabara na madaraja zitekelezwe na makandarasi wazawa na kusimamiwa na Washauri Elekezi Wazawa tu.
Kwa upande wa usimikwaji wa taa za barabarani, alisema TANROADS imepokea fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya kusimika taa za baraarani nchini kote.
Alitaja mikoa ambayo tayari imekwisha simikwa taa hizo kwenye baadhi ya barabara zake ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iriinga, Kagera, Kigoma, Kilimajaro, Lindi, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida, Songwe, Tabora, Tanga …
Aidha, alitaja uboresha miundombinu iliyoharibiwa na Mvua za El-Nino.
“Wakala imefanya kazi kubwa katika kurejesha hali ya miundombinu
baada ya kukumbwa na adha ya Mvua za El-Nino na Kimbunga
Hidaya,”alisema na kuongeza;
“Katika Ilani ya Chama, Daraja la Jangwani limesanifiwa na Mkataba
wake wa Ujenzi utasainiwa hivi karibu kabla ya Mwezi Agosti 2024
kuisha.
****Mafanikio mengine
Mlavi alisema jumla ya kilometa 15,343.88 zimekuwa kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji. Kwa mujibu wa Mlavi, kilometa 1,198.50 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Aidha, alisema kilometa 2,031.11 ziko kwenye hatua za ujenzi kwa kiwango cha lami. “Jumla ya Kilometa 2,052.94 na madaraja mawili yamefanyiwa upembuzi yakinifu tayari kujengwa kwa kiwango cha lami,”alisema.
Anataja mafanikio mengine kuwa jumla ya kilometa 4,734.43 na
madaraja 10 yapo kwenye hatua ya upembuzi yakinifu.
“Miradi ya Barabara yenye urefu wa Kilometa 5,326.90 na
madaraja saba ipo kwenye hatua ya upembuzi yakinifu na
usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi ya kujengwa kwa
kiwango cha lami,” alisema.
Alisema madaraja yaliyojengwa tisa Gerezani (Dar es Salaam).
Tanzanite (Dar es Salaam) Wami (Pwani) Kitengule (Kagera)
Kiyegeya (Morogoro) Ruaha (Morogoro). Ruhuhu (Ruvuma).
Mpwapwa (Dodoma) Msingi – Singida.
Alisema madaraja yanayojengwa ni matano Pangani (Tanga) J.P. Magufuli (Mwanza) Lower Mpiji (Dar es Salaam) Mbambe – (Pwani) Simiyu (Mwanza).
Kwa mujibu wa Mlavi, madaraja yatakayojengwa Godegode, Mtera –Dodoma. Ugala – Katavi, Kamshango, Kyabakoba, na
Kalebe – Kagera, Bujonde, Bulome, na Ipyana – Mbeya.
Chakwale, Nguyami, Mkundi, Mjonga, Doma, Mkondoa –
Morogoro, Lower Malagarasi – Kigoma. Sanga – Songwe.
Kilambo – Mtwara. Chemchem – Singida. Viwanja vya Ndege
Miradi saba (7) imekamilika
Julius Nyerere (Terminal Three), Mwanza, Mtwara, Songea,
Songwe (Runway), Songwe (Supply and Installation of
Airfield Ground Lights (AGL) na Geita .
Alisema miradi nane inaendelea ambayo ipo Msalato, Iringa, Musoma, Tabora, Shinyanga, Sumbawanga, Kigoma na Moshi.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best