Fresha Kinasa, TimesMajira Online,Musoma.
KIJANA Justine Mgaya mkazi wa Kijiji Cha Kaburabura Kata ya Bugoji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoa wa Mara amemshukuru Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kumsomesha kidato cha tano na kidato cha sita.
Justine Mgaya ambaye amehitimu kidato cha sita hivi karibuni katika shule ya Sekondari ya Nyakato iliyopo Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera amesema, kwake Prof.Muhongo ni sawa na Baba kwani alimsaidia mahitaji yote na kusimama naye kwa kila hatua.
Kijana huyo amewataka viongozi wengine nchini kuiga mfano wa Prof.Muhongo katika kuisaidia jamii na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutatua changamoto zao ili wapate maendeleo.
Ameongeza kuwa, baadhi ya vijana wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kutokana na familia zao kutokuwa na kipato cha kuwaendeleza katika vyuo mbalimbali ili wapate ujuzi ambao utawasaidia kujiajiri ama kuajiriwa.
“Namshukuru sana Prof.Muhongo kukubali kunipa mahitaji yote ya shule maana bila yeye mimi nisingehitimu kidato cha sita.Namuona sawa na Baba kwangu maana amenisaidia kurejesha na kuziishi ndoto zangu kwani hapo awali nilikata tamaa kabisa kwa habari ya kusoma.”amesema Justine.
Mathias Bwire ni Mkazi wa Kata ya Nyegina Wilaya ya Musoma amesema ni faraja kuona Mbunge huyo akiwashika mkono vijana wasiokuwa na uwezo kuwasaidia ambao baadae watakuwa msaadaa kwa jamii na taifa pia.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya