December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhariri Efm na Tv E ajitosa Ubunge Viti Maalum UWT

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam

MGOMBEA Ubunge wa Mkoa wa Dar es salaam Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Scholastica Mazula ambaye ni Mhariri Efm Radio na TV Eamechukua fomu ya kuwania kiti hicho leo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu na Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es salaam Grace Gama katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mazula amesema lengo kuu ni kushirikiana na kina mama katika kumsaidia Rais Dkt John Magufuli kuleta maendeleo nchini.

Scholastica Mazula amesema atahakikisha atashirikiana na Wana-CCM kusimamia ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika utekelezaji.