November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi:vyombo vya habari ni chachu ya maendeleo

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb)amesema kuwa waandishi wa habari ni chachu kubwa ya maendeleo kutokana na baadhi ya watanzania kutofahamu majukumu ya viongozi walinayo.

Hivyo kupitia vyombo vya habari kumekuwa msaada mkubwa wa kuwasemea mema viongozi na kufikisha ujumbe kwa wananchi .

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza katika mkutano mkuu wa chama cha waandishi Mkoa wa Mbeya (MBPC)

Amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakitoa taarifa za serikali za viongozi kwa watanzania ambao hawafahamu ratiba za kazi viongozi lakini kupitia vyombo vya habari wamekuwa wakipata taarifa mbali mbali za kazi zinazofanywa na viongozi wa kitaifa.

Mhandishi Mahundi amesema hayo Juni 14, mwaka huu wakati akizungumza na wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (MBPC) mara baada ya kutoa salamu kwenye mkutano mkuu wa chama hicho na kutekeleza ahadi yake ya milioni 1 ya Mbeya Press Club VICOBA.

“Mmekuwa mkitufanyia viongozi wote wema sana na hamkuangalia maslahi kwa kutoa taarifa za kazi mbalimbali za serikali ambazo zimekuwa zikifanywa na viongozi ,binafsi nafahamu nimefika hapa sababu ya vyombo vya habari labda watu wengi wasingeweza kuniona hata nilipokuwa Mkuu wa Wilaya kule Chunya bila vyombo vya habari hakuna ambaye angejua Chunya kunafanyika nini,”amesema Mhandisi Mahundi na kuongeza kuwa

“Bila vyombo vya habari nani atajua Rais yupo wapi anafanya nini , watanzania wengi hawafahamu ratiba za viongozi lakini kupitia nyinyi mmeweza kuhabarisha umma na kutusemea mema na kuwajenga viongozi,”.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya ,Nebart Msokwa

Mmoja wa wanachama wakongwe wa Chama cha Waandishi wa hyabari Mkoa wa Mbeya , Ulimboka Mwakilili alimwomba Naibu Waziri ziara maalum kwa waandishi wa habari wa mkoa huo ili kutembelea Bunge na kujifunza vitu mbali mbali ambavyo vitakuwa chachu kwao kwa masuala ya Bunge wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kihabari .

Kufuatia ombi hilo Mhandisi Mahundi alikubali na kuwataka waandishi hao wa habari kuanza maandalizi ya safari hiyo .

Mwenyekiti wa MBPC Nebart Msokwa amesema Naibu Waziri huyo amekuwa na ukaribu kwa waandishi wa habari hata katika utekelezaji wa majukumu yake .