January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi na Ridhwani kikwete watembelea Balozi ya Tanzania nchini Malawi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Malawi

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi(katikati)akiwa na Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete(kushoto) walipomtembelea Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedicto Mashiba(kulia)mara baada ya kumaliza mkutano wa Bonde la Mto Songwe walimtembelea ofisini kwake.

Mahundi ni Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo unaojumuisha nchi mbili za Malawi na Tanzania.

Lengo la mkutano mbali ya kuimarisha ujirani mwema ulikuwa na lengo la kudhibiti kuhama hama kwa mto Songwe sambamba na manufaa ya kiuchumi ili mto uweze kuzalisha mazao,kuondoa kero ya maji na kuzalisha nishati ya umeme.