Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya na Mkurugenzi wa Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF)ametekeleza ahadi yake ya kukabudhi mtambo wa kuchakata dhahabu (karasha)kwa Umoja wa Wanawake (UWT)Wilaya ya Kyela wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 na tofali 1350.
Hafla hiyo ya kukabidhi mtambo imefanyika Februari 2,2025 Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema katika kipindi cha Ubunge wake kiu yake ni kuona Wanawake wanafanikiwa kiuchumi huku akiishi kauli mbiu yake “Twende Tukue Pamoja”.
“Lazima tuhakikishe tunasimamia maono yetu, Mimi kama kiongozi nitahakikisha tunakuwa pamoja “amesema Mahundi.
Aidha amesema mtambo huo utawaongezea kipato wanawake wa Wilaya ya Kyela badala ya kutegemea mradi mmoja pekee.
Akipokea mtambo huo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kyela ,Secilia Mwakang’ata mbali ya kushukuru kupokea mtambo huo amesema Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amefanya mambo mengi kwa wanawake ikiwemo mitaji kwa wanawake,uwezeshaji wa majiko ya gesi kwa Mama Ntilie,miche ya matunda sanjari na kugharamia matibabu ya macho na saratani ya kizazi kwa wananchi Mkoani Mbeya katika kambi za Hospitali ya Mkoa na Wazazi Meta.
Katika hatua nyingine Mhandisi Maryprisca Mahundi amekabidhi tofali za saruji mia tatu hamsini na saruji mifuko thelathini na tano ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Wilaya ya Mbeya vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni tatu.
Amesema nyumba hiyo ikikamilika itasaidia Katibu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi pia mapokezi kwa wageni watakaotembelea Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Mbeya ,Beatha Wellah ameahidi kusimamia vifaa hivyo Ili vitumike kama ilivyokusudiwa.
Wellah amesema vifaa hivyo vitaongeza kasi ya ujenzi wa nyumba hiyo hivyo kuondoa kadhia ya kupanga.
Tangu Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi aingie madarakani baadhi ya miradi ya ujenzi wa nyumba za Makatibu wa Wilaya zinajengwa kwa kasi huku miradi mbalimbali ikiendelea kuimarika kutokana na ufuatiliaji mkubwa wa Mbunge lengo ni kuhakikisha Wilaya zote zinakuwa na miradi na nyumba za Makatibu.
Jijini Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi anaendelea na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya ambayo inagharimu zaidi ya milioni themanini.
Mbali ya uwezeshaji miradi ya Wilaya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewawezesha mitaji Wanawake mmoja Ili kukuza biashara zao.
.
More Stories
Rais Samia kupokea Tuzo ya ”The Gates Goalkeepers Award”
Walengwa wa TASAF watakiwa kujiandaa ukomo wa ruzuku
Kapinga:Azma ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika wakati wote