June 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mha.Mahundi:Rais Samia ataimarika vizur watumishi wakitimiza majukumu yao

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Chunya

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (MB) Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka watendaji wa chini kutekeleza wajibu wa kuzingatia misingi na weledi ili kumuwezesha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuimarika katika kuwatumikia watanzania.

Mhandisi Mahundi ambaye pia ni Mbunge viti maalum Mkoa wa Mbeya  amesema hayo Juni,16,2025 , aliposhiriki  kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya  Chunya cha kujadili hoja za  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Mkoa wa Mbeya ambapo mgeni rasmi  alikuwa Mkuu wa Mkoa w Mbeya ,Dkt.Juma Homera.

Mahundi amesema umefika wakati watumishi  kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kwa kuendelea kuchapa kazi kwa  mshikamano  hususani katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Tuendelee kufanya kazi bila kuchoka  ndugu zangu , Chunya imepata heshima kubwa sanaa kwa Rais Samia Suluhu Hassan”amesema Mhandisi Mahundi.

Wakati huo huo,amekipongeza Chama cha Mapinduzi(CCM), wilayani humo  kwa ushirikiano na serikali ndo sababu maendeleo yanasonga mbele na kulets  mabadiliko makubwa yanayo onekana .

“Nikiwa kama mkazi wa Chunya na Diwani ninaona namna mabadiliko ya maendeleo yalivyo makubwa niliishi kama Mkuu wa Wilaya mambo hayakua yalivyo leo hii majengo mengi na wananchi wameendelea kuwa na mwamko wa kujenga na Miji imekuwa kwakweli ninafurahi na ninajivunia kuwa mwana Chunya “amesema Mhandisi Mahundi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Dkt.Juma Homera amewataka madiwani kuendelea kumuunga mkono Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi .

“Ndugu yangu Mhandisi Mahundi amepambana sana juu ya mradi wa Maji wa Matwiga kwakweli mnatakiwa mpe heshima zake dada yetu mradi usingeweza kukamilika bila jitihada kwa kushirikiana na nyinyi na maendeleo hayaji tu ni kujitoa kwa watu kwa moyo “amesema Dkt Homera.