Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online -Mwanza
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamsaka Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Mgore anayekadirikiwa kuwa na umri wa miaka 25,mkazi wa Ibanda,Kata ya Kirumba, wilayani Ilemela,anasakwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza,kwa tuhuma za mauaji ya mume wake aitwaye Amosi Paulo(31).
Inadaiwa mwanaume huyo ambaye ni dereva pikipiki na mkazi wa Ibanda aliyeuawa na mtuhumiwa huyo( mke wake) kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani upande wa kisogoni.
Akizungumza mkoani hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Juni 25,2025, majira ya saa 4:30 usiku,katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure muda mchache wakati Amosi Paulo alipofikishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu,ili kufikia maisha yake.
Hiyo ni baada ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali na mke wake wakiwa chumbani kwenye nyumba ya Joseph Misungwi iliyopo eneo la Ibanda, Wilaya ya Ilemela walipokuwa wamepanga.
Mutafungwa amesema,wanaendelea na uchunguzi sambamba na kumsaka mtuhumiwa aliyetoroka baada ya kutenda tukio hilo ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Huku mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi.
Aidha, chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi, kwani inadaiwa mwanamke huyo alikuwa akimtuhumu mume wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengine.
Hata hivyo Mutafungwa ametoa wito kwa wananchi hasusani wanandoa, kutafuta suluhisho la migogoro kwa njia ya kisheria na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa viongozi wa dini, wazazi, ustawi wa jamii na vyombo vya usuluhishi badala ya sheria mkononi nakusababisha madhara kwa watu wengine.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi