Na Heri Shabani,TimesMajira,Online Dar
SERIKALI kuanzia kesho inatarajia kuanza rasmi ujenzi wa Barabara ya Vingunguti Barakuda wilayani Ilala.
Hayo yamesemwa na mgombea wa udiwani wa Kata ya Vingunguti kwa tiketi ya CCM, Omary Kumbilamoto wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani wa kata hiyo jana.
Pia ametumia nafasi hiyo kumuombea kura kwa mgombea urais wa CCM Rais John Magufuli na Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli.
“Kero ya barabara ya Vingunguti kuanzia Scania hadi Tabata Barakuda imepata ufumbuzi ujenzi wake unaanza mara moja kuondoa kero ya barabara hii, Rais John Magufuli ameshatoa sh. bilioni 2 za matengezo na kama fedha haijatosha atatoa pesa nyingine, kuhakikisha wananchi wa Vingunguti wanatumia barabara nzuri yenye kiwango,”alisema Kumbilamoto.
Kumbilamoto amewaomba wananchi Oktoba 28, mwaka huu kura zote ziende kwa CCM kwa Rais John Magufuli na Mbunge, Bonah Kamoli.
“Msifanye kosa tuchague viongozi hawa tuletewe maendeleo kwa kasi katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda,” amesema.
Amesema Serikali imetenga sh. bilioni 140 kwa ajili ya miundombinu Wilaya Ilala na Bilioni 32 kwa ajili ya Bonde la Msimbazi kwa ajili ya kuweka kingo mto huo.
Amewataka wamchague kwa ajili ya maendeleo ya Ilala na Vingunguti ambapo mara atakapochaguliwa atasimamia ujenzi wa mradi wa barabara za kisasa DMDP katika kata hiyo.
Aidha amesema katika kipindi chake cha miaka mitano ameweza kusimamia mradi wa serikali wa Machinjio ya Vingunguti ambapo kwa sasa upo katika hatua za mwisho.
Mradi huo umegharimu sh. bilioni 12 pia amesimamia sekta ya elimu kwa kuboresha elimu na mazingira ya shule na ujenzi wa sekondari.
Pia amesema mengine ambayo amefanya ni kuboresha setka ya afya ikiwemo kununua gari la wagonjwa la Zahanati ya Vingunguti na kuboresha Ofisi za CCM ndani ya Kata hiyo.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi