Na Mwandishi Wetu Timesmajira Online-Tabora
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya chama cha Wananchi CUF,Kapasha Haji Kapasha,ameomba wananchi wa Jimbo hilo kumpigia kura katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu,ili aweze kukomeshe vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma.
Kapasha ameahidi hayo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika uwanja wa taasisi, eneo la Soko Kuu Mjini hapa,ambapo amesema rasilimali nyingi za umma zimekuwa haziwanufaishi wananchi kutokana na usimamizi mbovu,ambao umesababisha Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kupoteza mapato mengi, hivyo akaahidi kuwa kama atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wao atayasimamia ipasavyo.

“Kama nitapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hili,ndani ya siku 100 za kwanza nitahakikisha mali zote za Manispaa zilizoibiwa au kumilikishwa kwa watu wengine zinarejeshwa haraka iwezekanavyo,”amesema Kashapa na kuongeza:
“Msifanye makosa, naomba mnichague kuwa Mbunge bunge wa Jimbo hili Oktoba 29 mwaka huu,ili nikawatetee bungeni na kuchochea mabadiliko ya kiutendaji katika halmashauri zetu kwani mambo mengi yanafanyika ovyo,”.
Sanjari na hayo amesema,viongozi wengi wanaochaguliwa wamekuwa wakifumbia macho mambo ya msingi ikiwemo kero za wananchi hali inayosababisha kushindwa kutatuliwa na kuongeza malalamiko zaidi.
Hata hivyo amesema,chama hicho kipo kwa ajili ya kutetea haki za wananchi hivyo amewahimiza kumchagua mgombea wa kiti cha Urais kupitia CUF,Gombo Samandito na wagombea Ubunge na Udiwani kwani hawatajuta.

Kwa upande wake mgombea Udiwani wa CUF Kata ya Chemchem,Nunu Ally,amesema Kata hiyo ipo nyuma kimaendeleo hivyo amewaomba wananchi wamoe ridhaa ya kuwa Diwani ili akasimamie maendeleo.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako