Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Mgombea Ubunge wa Jimbo la llemela kupitia chama cha CHAUMMA,Veronica Mgeta,ametaja vipaumbele saba ambavyo atavitekeleza endapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.
Veronica, amesema kipaumbele Cha kwanza ni afya ambapo atahakikisha jimboni humo kunakuwa na wauguzi WA kutosha,dawa na vifaa tiba muhimu.
Amesema kipaumbele cha pili ni elimu,ambapo akifanikiwa kuwa Mbunge, atahakikisha michango yote midogo midogo inaondolewa ili kurahisisha kila mtoto anapata elimu bora.
Pia amesema, kipaumbele chake cha tatu ni bodaboda na bajaji,ambapo atahakikisha wanakuwa na maeneo salama la kufanyia kazi bila kubuguziwa pamoja na kujenga chuo cha mafunzo na uendeshaji wa bodaboda na bajaji.
Aidha kipaumbele kingine ni machinga,ambapo atahakikisha wanatengewa maeneo yenye kufikiwa na watu na siyo kuwapeleka mahali ambako hakuna biashara pamoja na kuwawezesha kupata mikopo kwa ajili ya mitaji.
Kipaumbele kingine ni sekta ya uvuvi bapo atahakikisha anatetea haki za wavuvi ili wafanye kazi zao kwa usawa bila kubuguziwa.
Mbali na hayo pia kipaumbele kingine ni maji ambapo akifanikiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela,ata akikisja maeneo yote ya jimboni humo yanapata maji safi na salama.
Huku kipaumbele cha saba ni sekta ya ardhi,ambapo atatatua migogoro yote ya ardhi na kusimamia ulipwaji wa fidia wa haki.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako