Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
MGOMBEA kutoka Chama cha Alliance For Democratic Change(ADC),Wilson Mulumbe na Mgombea Mwenza Shoka Khamis Jume miongoni mwa wagombea wanaondelea kujitokeza katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC)kuchukua Fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kiti cha Rais na Makamo wa Rais.
Mulumbe na Mgombea mwenza walifika,jiji ni hapa leo ,Agosti 14,2025 Njedengwa zilipo ofisi za tume hiyo kikiwa ni chama cha 15 kuchukua fomu hizo ambapo baada ya kukabidhiwa alizungumza na waandishi wa habari huku akitaja vipaumbele vinne vya Chama hicho.

Ambapo amesema Kipaumbele chao cha kwanza ni Elimu bure kuanzia chekechea hadi Chuo kikuu lakini mara tu atakapo apishwa kitu cha kwanza ambacho atafuta ni makato ambayo wanakatwa wahitimu wa miaka iliyopoita kutoka kwenye tume ya elimu ya juu,
Huku akisisitiza”Nitafuta mara moja,
kwasababu hawa ni wataalamu na sisi kama ADC tutakuwa tukiwatumia,”amesema.
Kipaumbele chao cha pili ni Afya kuwa itakuwa bure na dawa zitakuwa bure kwa maana ya matibabu yote yatakuwa ni bure.
Ametaja Kipaumbele cha tatu kuwa ni huduma ya uungwanishaji wa umeme nchi nzima itakuwa ni bure ili kuweze kutoka kwenye asilimia 37 ya watu wanaotumia umeme hadi tufike asilimia 100.
“Hilo nitalifanya kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia nitakapo apishwa nitahakikisha kwamba Tanzania nzima itakuwa imeunganishwa na huduma ya umeme,”amesema.
Kipaumbele cha nne alitaja kuondoa gharama za uunganishwaji wa maji nchi nzima kuwa maji yatapatikana.
“Kwa Wilaya zile zenye changamoto kubwa za maji tutahakikisha kwamba serikali ya ADC itanunua magari yakuweza kuchimba visima ili tuhakikisha kila Mtanzania ataweza kupata huduma maji safi na salama.
“Lakini pia idara ya ustawi wa Jamii tutakuwa na Fao maalumu ambalo litakuwa linaitwa ‘Child Support Grand’,”amesema.
Vilevile amesema watatumia rasilimalinkama madini ili kila mzazi aweze kupata Fao la kumlea mtoto hadi atakapofika umri wa miaka 18.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako