December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgahawa unaotembea kuwainua vijana kiuchumi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

BODI ya Kahawa imezindua mradi wa mgahawa unaotembea maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ya watu ili kuweza kutoa huduma ya unywaji wa kahawa.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya 88 Nzuguni jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Primus Kimaryo amesema mkakati wao ni kuongeza unywaji wa kahawa kutoka asilimia 7-8 ambao ni unywaji wa sasa ,kwenda ailimia 15.

Amesema,imekuwa ni mazoea kwamba kilimo cha kahawa ndio wamiliki wa mashamba ya kahawa huku akisema bodi ikaona itafute namna ambavyo kijana anaweza kunufaika na zao la kahawa.

Amesema wamebuni mradi huo unaotembea ili kuwaweza vijana kujipatia kipato kupitia zao hilo la kahawa.

Kimaryo amesema mradi huo unawalenga vijana ambapo watapata mradi huo kwa mkopo nafuu na baada ya miaka mitatu muhusika anapaswa kurejesha gharama hizo za mkopo na mgahawa unakuwa ni mali yake.

Amesema vijana mbalimbali wameshaonesha nia ya kutaka kuwa na mgahawa huo .

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo msukumo mkubwa ni kuona namna gani vijana wanaweza kuoata ajira kupitia zao la kahawa kwani kijana kupata ardhi au kukodisha mgahawa ni changamoto.

Aidha amesema,mpaka hivi sasa gharama za mkopo huo ni shilingi milioni 30 huku akisema wanaanza kwa kutengeneza migahawa 100 kwanza ambayo pia itatengenezwa kwa awamu.

Amesema kabla kuoata mradi huo vijana wote wataokidhi vigezo vya kuoata mkopo huo ŵtapatiwa mafunzo ya uendeshaji wa migahawa hiyo ili iweze kuleta tija iliyokusudiwa.