Mwandishi wetu, YimesMajira,Omline Morogoro
WATAALAM wanaojenga mfumo wa Dirisha la Pamoja la Kuhudumia Wawekezaji la Kielektroniki Tanzania (TeIW) wamepongezwa kazi nzuri ambayo wanifanya katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa mfumo huu.
Wataalamu hao wamepongezwa na viongozi wa taasisi za serikali zinazotoa vibali, leseni na huduma mbalimbali kwa wawekezaji chini ya Kituo cha Mahala Pamoja (One Stop Facilitation Centre [OSFC]) baada ya mkutano wao katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma siku ya Jumatano.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ukauguzi huo wa viongozi, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Dkt. Maduhu Kazi, amesema kwamba viongozi wanaamini awamu ya kwanza ya ujenzi wa dirisha hilo utakwisha Februari 28 kama inavyotarajiwa.
“Tumeridhishwa na kufurahishwa na kazi ambayo tayari imefanyika. Tumewahimiza wataalamu wetu wandelee kwa kasi na ari ile ile ili tufikie lengo la kumaliza awamu ya kwanza tarehe 28, Februari,” amesema Dkt. Kazi. Ujenzi wa mfumo huo mpaka jana ulikuwa umefikia asilimia 42 ya utekelezaji.
Kiongozi huyo amefafanua kuwa Dirisha la Pamoja (Tanzania electronic Investment Window [TeIW]) ni suluhisho la mtandao ambalo linalenga kuwezesha na kurahisha upokeaji wa maombi, utoaji wa huduma za vibali, leseni na usajili kwa wawekezaji kwa haraka. “Lengo la mfumo huo ni kurahisisha mtiririko wa taarifa kati ya taasisi zote zilizoko ndani ya OSFC.”
Dkt. Kazi alieleza kuwa mfumo huo, ambao unafadhiliwa pia na Taasisi ya TMEA, utakuwa ni hazina ya taarifa zote muhimu kwa ajili ya uwekezaji kwa wadau wote wanaohitaji kuwekeza Tanzania na kuongeza kuwa utatekelezwa kwa awamu tatu ambapo kwa kuanzia utahusisha taasisi saba ambazo ni TRA, BRELA, Kazi, Uhamiaji, NIDA, Ardhi na TIC.
Jumatano, Kamati ya Kuhudumia Uwekezaji ya Taifai (NIFC), ambayo huhusisha taasisi za serikali zinazotoa vibali, leseni na huduma mbalimbali kwa wawekezaji, ilijadili maendeleo ya (TeIW) ilipokutana Dodoma katika Ofisi ya Waziri Mkuu na kuamua kuwatembelea wataalamu wanaojenga mfumo huo.
Dkt. Kazi alieleza kuwa NIFC imekuwa ni nguzo muhimu katika kutatua changamoto za wawekezaji na kuongezea kuwa kuna maboresho mengi ambayo TIC imeyafanya ikishirikiana na wadau ili kurahisisha utoaji wa huduma zote za vibali kwa wawekezaji.
“Lengo ni kuhakikisha kuwa tunakabiliana na changamoto zote za wawekezaji na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja kwa haraka ili wawekezaji waanzishe miradi yao katika kipindi husika bila kukwamishwa na huduma za taasisi zetu,” amefafanua Dkt. Kazi ambaye ni mwenyekiti wa NIFC.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi