January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mfumko wa bei wapungua, bidhaa zisizo za vyakula zachangia

Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

MFUMKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2022,  umepungua hadi asilimia 4.0% kutoka asilimia 4.2% kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba  mwaka jana.

Hiyo inamaanisha  kuwa ,kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari ,2022 imepungua ikilinganishwa  na kasi iliyokuwepo  kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba,2021.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini hapa, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii  wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja ametaja baadhi ya  bidhaa zisizo za vyakula  zilizoonesha kupungua kwa mfumuko wa bei  ambavyo ni pamoja na  mavazi  kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia 2.8%,viatu kutoka asilimia 4.6% hadi asilimia 4.4%.

Bidhaa nyingine zilizosababisha kupungua kwa mfumko ni kodi ya pango  kutoka asilimia  4.4%  asilimia 1.2%.magodoro kutoka asilimia 12.3%hadi asilimia 7.3%,majokofu kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 1.5%,cherehani kutoka asilimia 9.1% hadi asilimia 5.0%, simu janja kutoka asilimia 3.5 hadi asilimia 3.3%.

 Aidha Minja ametaja bidhaa nyingine kuwa ni vyombo vya nyumbani kama sahani kutoka asilimia  kutoka asilimia 16.7%  hadi asilimia 3.6% ,luninga kutoka asilimia 3.5% hadi asilimia 1.2% na malazi kwenye hoteli  na nyumba za kulala wageni kutoka asilimia 6.6%  hadi asilimia 2.9%.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema ,kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Mwezi Januari ,2022   kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumko wa bei wa baadhi  zisizo za vyakula  kwa kipindi kilichoishia mwezi Januari ,2022  ikilinganishwa na kipindi kilichoishia mwezi  Disemba 2021 .

Amesema,mfumko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi  kwa mwezi Januari ,2022  umepungua kwa asilimia 3.1%  kutoka asilimia 3.9% kwa ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2021 huku mfumko wa bei ambao haujumuishi vyakula visivyochakatwa ,nishati na bili za maji kwa mwezi Januari  2022  umepungua hadi asilimia 3.3% kutoka asilimia 4.6%  ilivyokuwa mwezi Disemba mwaka jana .

Akitaja hali ya mfumko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki Minja amesema,kwa nchi ya Uganda  umepungua hadi asilimia 2.7% kutoka asilimia 2.9 % huku nchini Kenya  ukipungua  kutoka asilimia 5.39 % kutoka asilimia  5.73.