January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya Kumbilamoto aipongeza NHC kutatua kero ya Machinjio

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam omary Kumbilamoto amepongeza Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba ( NHC) kutatua kero Machinjio ya Vingunguti .

Meya Kumbilamoto alitoa pongezi hizo leo wakati wa ZIARA ya watendaji wa Shirika la Nyumba NHC waliofanya katika Machinjio hayo na Watumishi wa NHC.

Akizungumza katika ziara hiyo Meya Kumbilamoto alimpongeza Mkurugenzi wa NHC Nahemiah Mchechu kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo .

“Nakupongeza Mkurugenzi wa NHC leo umeweza kufika Vingunguti katika Machinjio ya kisasa kuja kutatua kero mbalimbali kwa kuambatana na Watendaji wa Halmashauri ya Jiji na Wakuu wa Idara wa NHC “alisema Kumbilamoto.

Meya Kumbilamoto alisema dhumuni la Ziara hiyo Watumishi wa Shirika la Nyumba na Mkurugenzi wao kuja kutatua kero katika mradi wa Machinjio ya kisasa Meya Kumbilamoto alitaja baadhi ya kero zilizotatuliwa katika ziara hiyo leo ni uwekaji wa viyoyozi katika jengo zima na umaliziaji wa ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Vingunguti .

Katika hatua nyingine Meya Kumbilamoto alipongeza Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Jiji kwa ushirikiano wao na usimamizi Bora wa Mradi .