December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya Kumbilamoto agawa sembe kwa wazee 500

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ameaga mwaka 2021 kwa kugawa sembe kwa wazee Wajane 500 waliopo Vingunguti Wilaya Ilala.

MEYA Kumbilamoto aligawa misaada hiyo leo Desemba 30/2021 kwa wajane 500 sehemu ya utaratibu wake aliojiwekea katika kusaidia makundi maalum na kukaribisha mwaka 2022.

“Misaada hii ya chakula imetolewa na WADAU wa Maendeleo Agro Premium ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia jamii ” alisema Kumbilamoto.

MEYA Kumbilamoto alisema kampuni hiyo ya Agro Premium pia inawalisha Wanafunzi elfu kumi wa Wilaya Ilala

Kumbilamoto alisema misaada hiyo utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika utatuzi wa kero.

Amewataka viongozi na Wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi zake katika kuwasaidia wananchi kwa kutatua kero zao.