Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodma
WABUNGE na watumishi wa Bunge waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wameaswa kuisaidia Serikali kukemea vitendo vya uzembe kazini,matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana kwani ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwajibikaji,uhodari, uzalendo, ukakamavu na stadi za maisha.
Mkuu wa Utumishi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Paul Simuli,ameyasema hayo Agosti 5 mwaka huu wakati akifunga mafunzo ya awali ya JKT, Oparesheni Jenerali Venance Mabeyo, kundi maalum la wabunge na watumishi yaliyofanyika kikosi 834 KJ Makutopora jijini Dodoma.
Amesema kitendo cha kuhudhuria mafunzo hayo kunawafanya kuwa wakakamavu, wazalendo, watii na wenye Moyo wa utayari wa kufanya kazi katika mazingira yoyote na nina amini mara baada ya kurudi majimboni utandaji kazi utabadilika.
Amesema,mafunzo hayo yakawe chachu katika utendaji wa kundi hilo kwa kukemea vitendo ambavyo vimekuwa vikiathiri nguvu kazi ya Taifa.
Ametumia nafasi hiyo kulishukuru kwa kuwapa nafasi wabunge na watumishi kuhudhuria mafunzo hayo ikiwa ni hamasa kwa vijana kuhudhuria mafunzo hayo na kuzitaka taasisi nyingine kuwapeleka watumishi wao ili wapate mafunzo hayo na kujenga uzalendo na mshikamano kazini kwa maendeleo ya taifa.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kuendelea kujilinda na maambukizo ya UVIKO-19 kwa kufuata taratibu zote zinazoshauriwa na wataalam wa afya.
“Covid-19 ndugu zangu bado ipo hivyo hatunabudi kuendelea kuchukua tahadhari lakini pia nawashauri kujitokeza kwa wingi kushiriki sensa ya watu na makazi itakayo fanyika mwishoni mwa mwezi huu”amesema
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kanali Erasmus Bwegoge amewashukuru wabunge waliojitoa kupata mafunzo hayo na kuwapongeza wakufunzi wa mafunzo na wanaamini kwa paredi waliyopiga mafunzo hayo yamewaingia.
Amesema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia katika kuwa wazalendo na wavumilivu katika majukumu yao hasa katika kutunga sheria na katika kuwawakilisha wananchi wao Bungeni.
Awali Mkuu wa kikosi cha 834 KJ Makutopora Dodoma Luteni Kanali Festo Mbanga amesema kozi hiyo imepewa jina la Oparesheni Generali Venance Mabeyo ili kuenzi kazi nzuri aliyoifanya mkuu wa majeshi ya ulinzi mstaafu.
Amesema kuwa mafunzo hayo yalikuwa ni ya majuma manne ambayo yalianza julai 5 hadi august 5, 2022 yakihusisha watumishi na wabunge 39.
“Katika kozi hii tulikuwa na wanafunzi 39, ambao wote wamemaliza mafunzo wabunge walikuwa 21 na watumishi wa bunge ni 18 ambao tumefundisha, uzalendo, ujasiri, stadi za kazi, usomaji ramani, ujanja wa polini, kufunga na kufungua siraha, mbinu za kivita, ushujaa, kwata,histori ya JKT na JWTZ”amesema
Naye Mbunge wa Iringa mjini, Jesca Msavatavangu, akisoma risala ya kuhitimu mafunzo ya awali ya JKT, Oparesheni Generali Venance Mabeyo, kundi maalum la wabunge na watumishi,ameishauri serikali kutafuta mfumo ambao utatumika kwa wateule wa Rais kupatiwa mafunzo ya JKT, ili kuwasaida kuwa wazalendo na Taifa lao na kufanya kazi kwa uadilifu.
“Tunapendekeza bunge kuishauri serikali kuona namna ambayo mafunzo haya tuliyoyapata leo iwe ni kitu cha muhimu kwa wateule wa Rais kukipata ili kuwasaidia kujifunza uzalendo na kulipenda Taifa lao”amesema
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best