Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
WAKATI joto likizidi kupanda kuelekea mchezo wa Watani wa Jadi, Yanga na Simba uliopangwa kuchezwa Oktoba 18, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko na kusogeza mbele mchezo hhuo hadi Novemba 7, 2020.
Licha na ya mchezo huo namba 61 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kusogezwa mbele lakini utachezwa muda ule ule uliopangwa awali katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 7, 2020 na Idara ya Habari na Mawasiliano, imesema kuwa, mabadiliko hayo yametokana na uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa vikwazo katika usafiri wa kimataifa baada ya kukamilika kwa michezo ya kimataifa iliyo kwenye kalenda ya FIFA jambo ambalo linaweza kuathiri vikosi vya klabu hizo mbili.
“Nchi mbalimbali bado zimeendelea kuweka masharti magumu katika taratibu za usafiri wa kimataifa tangu kuzuka kwa janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19,” imeeleza taarifa hiyo.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM