Joyce Kasiki,Timesmajira online Dodoma
MBUNGE wa Kwela Deus Sangu (CCM) ameihoji Serikali kwamba ina mkakati gani wa haraka wa kujenga madaraja yaliyoharibika katika Jimbo la Kwela.
Mbunge Sangu ametoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la msingi Bungeni jijini Dodoma ambapo katika maswali yake ya nyongeza Mbunge huyo aliitaka kujua mpango wa Serikali wa kujenga barabara inayounganisha Kata ya Lusaka na vijiji vyake kwa maana ya barabara ya Ndelema kwenda Mpembano hadi Kamzacha huku akisema barabara ya kutoka Lusaka kwenda Kazumbi zina hali mbaya.
Pia alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara ya Liwevula hadi Kapenta gente mrefu wa kilomita 15 na ina hali mbaya na ni barabara ya kimkakati kwa ajili ya uchumi hasa wa kilimo Cha mpunga na hivyo kutegemewa na wakulima hasa kipindi cha mavuno kwa ajili ya kusafirisha mazao yao.
Akijibu masaaki hayo,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainabu Katimba amesema kuwa Serikali itatafuta fedha za kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko.
Kwa mujibu wa Katimba ,katika mwaka 2024/2025 Serikali imetenga shilingi milioni 167 ambapo Daraja la Mfinga katika Barabara ya Mfinga – Kasekela hadi Msila lililoharibiwa na mvua litajengwa.
Aidha amesema,Serikali imetenga fedha za dharura kwa ajili ya kurejesha mawasiliano katika maeneo yaliyokatika na mvua za El nino zilizonyesha kuanzia Oktoba 2023 hadi mwaka huu 2024 ambapo Jimbo la Kwela limepata shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Kasekela (Upinde wa Mawe) katika Barabara ya Mfinga – Kasekela – Msila.
“Sambamba na hili, usanifu wa daraja la Ilembo katika Mto Nyinaluzi umekamilika na limekadiriwa kugharimu shilingi bilioni 1.35 ambapo ujenzi wake utaanza pindi fedha we fx how, ” alisema Katimba.
Amesema kuwa Serikali inaendelea na usanifu wa Daraja moja la Chitete katika barabara ya Chitete – Chisungamile na madaraja matatu ya Mnokola 1, Mnokola 2 na Mititi 1 katika Barabara ya Mnokola – Mititi – Mombo ambapo baada ya usanifu kukamilika.
Akijibu maswali ya nyongeza Katimba alianza kwa kumpongeza Mbunge huyo kwa kuwa amekuwa akifuatilia kwa ukaribu maendeleo ya miundombinu ya barabara katika Jimbo lake.
Aidha amesema barabara ya Ndelema Kamnyazya katika mwaka wa fedha 2023/2024 serikali ilitenga milioni 63.139 ambapo ilijenga Kilometa 9 na Kilometa 2.5 ziliwekwa changarawe na kwamba kalvati moja lilijengwa na mtaro wa mita 200.
“Katika mwaka wa fedha 2023/2024 serikali ilitenga milioni 22.26 kwa ajili ya kutengeneza barabara ya Lusaka Kizumbi kwa urefu wa Kilometa nne na kwamba katika mwaka wa fedha 2024/2025 serikali ilitenga milioni 35.2 kwa ajili ya kuendeIea kurekebisha barabara hiyo na hasa matengenezo ya kipande cha Ndelema Kamnyazya.
“Naomba ni mhakikishie mbunge serikali inaendelea kutoa fedha kuhakikisha inarekibisha miundombinu hii,” amesema Katimba.
Kuhusu barabara ya Liweliavula Kata ya Kapenta yenye Kilometa 15.7 Katimba amesema,katika mwaka wa fedha 2024)2925 serikali imetenga milioni 400 kwa ajili ya kufungua na kutengeneza kwa urefu wa Kilometa 5.8 ikiwa ni awamu ya kwanza na kwamba marekebisho hayo yatafanywa katika kijiji cha Kikwale
“Serikali inajua umuhimu mkubwa wa barabara hasa katika kipindi cha Kilimo cha mpunga na itaendelea kutenga fedha kuhakikisha inaboresha miundombinu ili kutokwamisha uchumi wa wananchi kwenye shughuli za kilimo.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato