December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline, Mbarali

MBUNGE wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, Bahati Ndingo amesema kuwa Chama cha Mapinduzi(CCM)kimejipambanua vizuri pamoja na kujidhatiti katika kuwaletea  maendeleo wananchi wake.

Amesema kuwa kwa wilaya ya Mbarali takwimu zinaonyesha chama cha Mapinduzi kimesimamisha wagombea kwenye vijiji vyote 112 na vitongoji wagombea 712.

Ndingo amesema hayo Novemba 21,2024 wakati wa ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika kata ya ubaruku  kijiji cha Utyego wilayani Mbarali  mkoani hapa.

“Ndugu yangu MNEC nimepita kwenye vijiji zaidi ya 90,kati ya vijiji 102 vya wilaya hii na vitongoji 612,  kati ya vitongoji 712, vilivyopo wilaya hapa  nimeona wagombea ni majembe ya kazi nimezunguka nao wapo vizuri  na wana uwezo mkubwa,naomba tusiangushane tuleteeni wenyeviti wanaotokana na Chama cha Mapinduzi ili kiweze kuwaletea maendeleo “amesema Mbunge Ndingo.

Akielezea zaidi Ndingo amesema kwamba CCM ni chama pekee ambacho kinafanya kazi zake kwa mipango na utaratibu maalum na kuomba wananchi kuendelea kukiamini chama hicho na kwamba changamoto nyingi walizozikuta zinaendelea kufanyiwa  kazi.kwa vitendo.

Kwa upande wake Mjumbe wa halmashauri kuu CCM  Taifa kupitia mkoa wa Mbeya (MNEC)Ndele Mwaselela amewapataka wagombea wa nafasi za uenyekiti wa vitongoji na vijiji wilayani humo kufanya Kampeni za kistaarabu pasipo kutukana watu na kuonyesha namna chama cha Mapinduzi kilivyowalea.

“Wao watakuja na kuwapalua nyie msiwapalue badala yake muwabatize kwa Lugha ya upendo kwasababu wapo huko kwa muda watarudi muda sio mrefu ,Mh Bahati Ndingo anafanya kazi kubwa maana nimeona anafanya ziara sasa mpeni hawa wasaidizi wake ili akafanye ziara kwenye vijiji na vitongoji awe na nguvu zaidi “amesema Mwaselela.

Mary Mbwilo ni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbarali amesema kuwa wana kazi kubwa ya kuweka historia kata ya ubaruku.