Na Mary Margwe, Hanang’
MBUNGE wa Viti Maalum mkoani Manyara, Regina Ndege ametatua changamoto ya watoto wenye uhitaji katika Shule ya Msingi Katesh A wa kitengo maalum kwa kutoa msaada wa viti mwendo viwili, magongo ya kutembelea mawili, kofia 10 kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, mafuta 10 pamoja na miwani ya kuzuia jua 10, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh. milioni 3.
Msaada huo ameukabidhi mbele ya mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Katesh A, Martida Shio, Afisa Elimu Maalum Wilaya ya Hanang’, Albert Machua huku akiambanata na Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Wilaya ya Hanang’, Scola Kipendi Simba, madiwani wa viti maalum Tarafa ya Katesh, Jully Songay na Isabela Gabriel.
Ndege amesema, msaada alioutoa kwa watoto hao ulitokana na kupatiwa changamoto ndipo akajipanga na hatimaye kuweza kufanikiwa kutoa kwa wanafunzi waliokua na uhitaji wa vifaa hivyo.
“Kama tunavyofahamu zipo changamoto nyingi, isipokua huwa zinazidiana, hivyo nilipoambiwa changangoto ya watoto hawa ilinigusa sana nikaona nijipange kutafuta kwa bidii vifaa hivi na namshukuru Mungu leo nimekuja kukamilisha hili zoezi la kutoa vifaa hivi, ambapo kwa kundi hili nimemaliza,”amesema Regina Ndege.
Aidha, amesema kwa sasa atakwenda kujipanga kadri atakavyofanikiwa kwa ajili ya watoto wasiosikia ( viziwi ) , wasioona, wenye ulemavu wa akili hao atahakikisha anaendelea kuwapambania kadri atakavyojaliwa ili aje aende kuwaona kama ambavyo amewaona hao wengine.
Aidha, Mbunge huyo ameahidi kwenda kuwasemea wanafunzi hao bungeni, hasa ukizingatia kitaaluma Mbunge huyo ni mwalimu, licha ya kuwa wanafunzi walemavu wanatambuliwa na serikali, hivyo ana imani kuwa Wizara ya Elimu itatenga bajeti kwenye elimu maalum.
Kufuatia utoaji wa vifaa hivyo, Mbunge huyo pia alitumia fulsa hiyo kuwataka wadau mbalimbali kuweza kujitokeza kuendelea kutatua baadhi ya Changamoto zilizopo katika shule hiyo na zinginezo ili walimu na wanafunzi waweze kutimiza ndozo za ufundishaji na usomaji kwa wanafunzi kikamilifu, huku akiishukuru serikali kwa kuanzisha na kuhudumia shule hiyo ya kitengo maalum ambayo inawaongezea uwepo wa wqnafunzi kupata elimu.
Kufuatia msaada huo mmoja wa wanafunzi hao, Jackson Morson ambaye ni mlemavu macho amemshukuru Mbunge huyo Kwa kuwatembelea lakini kikubwa kuwasaidia vifaa vitakavyowawezesha kuwasaidia kutimiza hitaji la kila mmoja wao.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo, Martida Shio amemshukuru Mbunge Regina kwa jitihada zake za kuwasaidia wanafunzi hao vifaa hivyo, ambavyo ni muhimu kwa kila mwenye hitaji, huku aliwataka wadau wengine kuiga mfano huo.
Hata hivyo, Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Wilaya ya Hanang’, Scola Kipendi Simba, Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Katesh Juliana Songay, Isabela Gabriel wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuweza kuwafikia na kuwasaidia wanafunzi hao wenye uhitaji huo.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam