Na Doreen Aloyce, TimesMajira Online, Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali, amesema kipigo alichopata Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe jijini Dodoma kimetokea kutokana na kulewa pombe.
Lijuakali ametoa madai hayo Bungeni leo wakati alipokuwa akichangia azimio la kumpongeza Rais, Dkt. John Magufuli kwa jitihada za kupambana na ugonjwa wa Corona.
Amesema, Mbowe na wenzake wakiwemo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walikuwa wamelewa hivyo aliteleza na kudondoka kwenye ngazi nyumbani kwake na kuvunjika mguu na sio kupigwa na kukanyagwa kama anavyodai ameshambuliwa na wasiojulikana.
“Kuwa kiongozi mkubwa wa CHADEMA inakuwaje atembee mwenyewe bila walinzi ilihali wapo? hivyo anataka kuisingizia Serikali kwa masuala ya kisiasa,” amesema Lijualikali na kuongeza;
“Naomba mfahamu hii michezo inafanyika na ni usanii na cha kujiuliza kwa nini aende hospitali ya Ntyuka na sio General Hospotali ya Serikali kwa kuhofia kupimwa ili asionekane kama amelewa,”ameongeza.
More Stories
Rungwe yajenga soko kukuza uchumi kwa wananchi
Waislamu Mwanza wapokea Ramadhani kwa maandamano ya kidini
Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala,katiba na sheria yaridhishwa ujenzi soko Kariakoo