Na Doreen Aloyce, Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Pangawe Haji Amri Haji amesema ili taifa liweze kusonga mbele kiuchumi lugha ya kiswahili inapaswa kukuzwa huku akiitaka sekta ya elimu kubadilka katika ufundishaji wa lugha .
Mbunge Haji ametoa kauli hiyo Katika viwanja vya Bunge wakati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya bajeti ya elimu kwa mwaka 2023/2024 ambayo imepitishwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa nchi nyingi za Ulaya zilizoendelea hususani nchi ya Russia na China zimekuwa zikitumia lugha zao kwa sababu ya mfumo wa kibiashara na kiuchumi ambapo hali imechangia kuwa na mafanikio makubwa .
“Ninachotaka kumanisha ni kwamba kwa sisi Tanzania tunapaswa kubadilika katika ufundishaji wa lugha kwa kuchanganya lugha mbili ya kiuchumi na lugha ya ufaulu ambapo katika ufaulu mtu anaweza kujifunza lugha kwa namna yoyote,”amesema Haji na kuongeza kuwa
” Mimi binafsi nina mawazo kwamba ili nchi iweze kuendelea tunapaswa kuwa na lugha mama ya kiswahili na kama tunataka lugha ya ufaulu tungechanganya lucha zote sio kiingereza tu hata kifaransa na lugha nyunginezo,” amesema Mbunge Haji.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini