November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge CCM adaiwa kukamatwa na bunduki 10

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Masoud Suleiman maarufu kwa jina la Nchambi akituhumiwa kwa kosa la kupatikana na silaha na nyara za Serikali kinyume na sheria.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba, amewaambia waandishi wa habari leo kuwa, mbunge huyo alikamatwa Mei 3, mwaka huu saa 5.45 usiku katika Mtaa wa Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Akifafanua zaidi Kamanda Magiligimba amesema mbunge huyo alikamatwa na silaha 16 pamoja na risasi 536 nyumbani kwake eneo la Lubaga ambazo zilikuwa zimehifadhiwa ndani ya kabati la nguo.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kati ya silaha hizo, 10 alikuwa anazimiliki isivyo halali.

Amesema, mtuhumiwa anatuhumiwa kujihusisha na uwindaji haramu katika eneo la Negezi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.760 DSD aina ya Nissan Hardbody, ambapo katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwake kulikutwa na kilo 35 za nyama inayohisiwa ni ya wanyamapori ilikamatwa ikiwa imeihifadhiwa kwenye jokofu jikoni.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Majira kesho