November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Bonnah atoa donge nono katika mashindano ya Kumbilamoto cup

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,amesema mshindi wa kwanza wa mwaka huu katika mashindano ya Kumbilamoto Cup atamzawadia shilingi milioni 1 taslim na mahindi wa pili atampa shilingi 500,000/= na mshindi wa tatu atampa shilingi 300,000/=

Mbunge Bonnah ,amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mpira wa miguu ya Kombe la Kumbilamoto Cup yalioshirikisha Timu 20 kutoka Vingunguti.

“Mpongeza Meya wa Jiji Omary Kumbilamoto kwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuunganisha vijana katika sekta ya michezo kwani michezo ni afya,ajira pia ujenga mahusiano na udugu na uwafanya vijana wawe bize katika mpira”alisema Bonah.

Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli ,amesema pesa hizo anazoongeza katika shilingi milioni 1.8 akiwa safari atamkabidhi Katibu wake kuziwasilisha katika Fainali ya mashindano hayo .

Katika hatua nyingine alimpongeza Meya Kumbilamoto kwa kuleta maendeleo kwa wananchi wake wa Vingunguti amewataka wananchi wa Vingunguti mwaka 2025 kumpigia kura Diwani wao Meya Kumbilamoto ili aweze kuwaongoza tena ..

Mratibu wa mashindano hayo ya Kumbilamoto Cup Meya wa Halmashauri ya jiji Omary Kumbilamoto alisema jumla ya timu 20 zinashiriki mashindano hayo ambapo mshindi wa kwanza atapewa Ngombe medali 25 kikombe mipira mitatu.

Omary Kumbilamoto alisema mshindi wa pili atapewa mipira miwili ,mbuzi ,medali 25 mshindi wa tatu mbuzi,mipira na mshindi wa nne mipira miwili.

Aliwataka vijana kushiriki michezo kwani michezo ni afya,ajira pia vipaji mbali mbali vinapatikana katika sekta ya michezo.

Mwenyekiti wa Mashindano ta Kumbilamoto Cup Mohamed Mwarabu mashindano hayo yameandaliwa na Kuzaminiwa Kumbilamoto Foundation na Tandika Plaza dhumuni kuwaweka vijana pamoja na kuwatengezea ajira kupitia michezo.

MWENYEKITI Mohamed Mwarabu alisema pia mashindano hayo mchezaji bora atapewa kiatu na jezi , mchezaji wa pili kiati na jezi ,golikipa bora Grops, kikundi cha Hamasa shilingi 100,000/= Shabiki bora shilingi 50,000.