November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Bonnah agawa jezi za mashindano ya Bonah Cup 2024

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MBUNGE wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus, amegawa jezi za mpira wa miguu kwa ajili ya mashindano ya Bonah Cup 2024 kwa timu 61 za jimbo la Segerea .

Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli .akigawa jezi hizo kwa mitaa 61 ambayo inashiriki mashindano hayo ya mpira wa miguu kwa Wanaume na Rede ya wanawake.

Akigawa Jezi hizo Mbunge Bonnah alisema ufunguzi wa mashindano hayo yanatarajia kufanyika April 4 mwaka huu katika uwanja wa TABATA shule wilayani Ilala mkoa Dar Es Salaam.

“Nimegawa jezi kwa timu 61 za jimbo la segerea kwa ajili ya mashindano ya Bonah Cup mwaka 2024 ili timu zote ziweze kushiriki mashindano haya bure hayana kingilio ambayo yanafanyika kila mwaka kwa kushirikisha timu zote za Segerea michezo hii ujenga Afya Ajira naomba timu zote shiriki ziweze kufuata taratibu na sheria”alisema Bonnah.

Mbunge Bonnah aliteuwa Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala isimamie michezo ya wanawake Rede ambapo kazi hiyo alimkabidhi Mwenyekiti wa umoja UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa.

Wakati huo huo Mbunge Bonnah alitangaza zawadi za Bonnah Cup 2024 mshindi wa kwanza kwa mpira miguu shilingi milioni 5 mshindi wa pili milioni tatu na mshindi wa tatu milioni 2..

Aidha pia alitaja zawadi za mashindano ya Rede Cup jimbo la Segerea mshindi wa kwanza milioni 2 mshindi wa pili milioni 1 na mshindi wa tatu wa Rede shilingi 500,000/=

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ilala Neema Kiusa alimpongeza Mbunge Bonnah kuratibu mashindano hayo ambapo alisema UWT itasimamia vizuri na kutenda haki.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Ilala Juma Mizungu alisema UVCCM itaendelea kutangaza mazuri ya Jimbo la Segerea, UVCCM ipo imara na timu za vijana wote .