November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge aunga mkono mjadala nishati safi ya kupikia

Na  Penina Malundo,timesmajira

MBUNGE  wa Jimbo la Iringa mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Nishati  na Madini,Jesca Msambatavangu ameunga mkono kauli ya  Rais Samia Suluhu Hassan ya ifikapo mwaka 2032 asilimia kubwa ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia na kudai kuwa lazima ifike mahali Watanzania kwenda na kasi na  mabadiliko ili kuweza kunusuru Majanga mbalimbali ya Kiafya na Kimazingira. 

Akizungumzia hayo leo Jijini Dar es Salaam ikiwa siku ya pili ya Mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati,Msambatavanga alisema Watanzania waanze kufikiria namna ya kutumia nishati safi ya kupikia kwani endapo wataendelea kutumia nishati Chafu  ya kupikia inauwezo wa kuleta athari kubwa za kiafya.

Amesema mbali na athari za kiafya pia inaweza kuathiri kwa kiasi kikuwa uchumi wa nchi kutokana na kuathirika kwa mazingira ambapo watu ukata miti hovyo.”Tukiwa na ukame shughuli zetu za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi zitakuwa haziendelei huku asilimia 80   ya Watanzania wanafanya shughuli  hizo hivyo miti ikiendelea kukatwa nchi itapelekwa katika jangwa,”amesema na kuongeza 

“Naungana na Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Makamba kuwa ifikapo 2032 tuhame kutumia nishati safi ya kupikia,Iringa ni moja ya mkoa mmoja wapo inayokata miti sana ila angalau tunakata miti ya asili na kupanda miti ya kisasa,”amesema

Amesema lazima watu wakubali kwendana na mabadiliko uwezi kusema tutabaki katika kutumia nishati ya Kuni na Mkaa ni lazima kuwepo kwa madiliko.” Kadri siku zinavyozidi kwenda lazima tubadilike na suala hili sio suala la gafla itafika tu mahali Watanzania tutabadilika na endapo tukikubali tunapoelekezwa na wataalam,”amesema