March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge atoa Jenereta Kanisa Katoriki Ilembo

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

UONGOZI wa Kanisa la Mtakatifu Yakobo  Mtume Parokia ya Ilembo umepokea Genereta lenye thamani ya shilingi laki Nane kwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini,Oran Njenza kwa ajili ya waimbaji  wa Kwaya za Familia Takatifu na  Kwaya ya Mtakatifu Agustino.

Imeelezwa kuwa Jenereta hilo ni ahadi ya Mbunge Njeza ambayo alitoa hivi karibuni kwa kanisa Katoliki ili liweze kusaidia shughuli za uimbaji wa Kwaya kanisani hapo.

Mchango huo Sadaka umekabidhiwa  Juni 22,2025  na katibu wa Mbunge , Peter Mtepa  kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini,Oran Njenza na kupokelewa na wanakwaya wakiongozwa na paroko wa Parokia hiyo Padri Stephano Gindo.

Akizungumza na mamia ya waumini wa kanisa hilo amesema huo ni mwendelezo wa Mbunge kutekeleza ahadi ambayo walimwomba alipofanya ziara katani humo (Ilembo) kama ambavyo amekuwa akitekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kwenye nyumba za ibada jimboni kwake.

Amesema kuwa Jenereta hilo ni kwa ajili ya kwaya hizo zinapoenda kuhubiri katika maeneo mbalimbali na kanisa kwa ujumla kama walivyoahidiwa na Mbunge Njeza baada ya kumuomba msaada wake miezi miwili iliyopita ambapo pia aliwanunulia na kuwakabidhi kinanda cha kisasa.

Pamoja na hayo Mbunge Njeza amekabidhi mchango wake wa shilingi laki tano kwa ajili ya shughuli ya upadirisho wa mtumishi wa Mungu Eneliko Mwamwezi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2025 katika kanisa la Roman Catholic Parokia ya Ilembo.

Akizungumza mara baada ya kupokea Jenereta hilo ,Paroko wa Parokia ya Ilembo Stephano Gindo, amemshukuru Mbunge kwa kuwa na moyo wa upendo na kujali watu wake na kuchangia sadaka kwa ajili ya upadirisho huku nao waimbaji wakiahidi kumwombea kwa Mungu kiongozi huyo kwa mchango wake katika kuinua uinjilishaji.

“Tunashukuru kwa msaada huu kwa Mbunge Njeza kwani utakuwa msaada mkubwa kwa Kwaya zetu hizi “amesema Paroko.