December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge agawa majiko 150 Soko la Kisutu

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

MBUNGE wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, amegawa majiko ya gesi 150 Bure kwa Mama lishe na Baba Lishe wa soko la Kisutu wilayani Ilala .

Mbunge Zungu aligawa majiko ya Taifa gesi soko la Kisutu Leo kwa Wajasiriamali wa soko hilo mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija .

Akizungumza wakati wa kugawa majiko ya gesi ya Taifa gesi Mbunge Zungu alisema kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan, kumtua Mzigo wakuni mama Kichwani katika kata ya Kisutu Jimbo la Ilala nimetekeleza .

“Hivi Karibuni nchi yetu ilikumbwa na janga Wananchi wanateseka na maji ,maji ni uhai bila maji uwezi kuoga wala kupika wala kufanya Shughuli yoyote ya kijamii “alisema Zungu.

Mbunge Zungu alisema gharama ya nishati ya mkaa ni kubwa amewataka mama lishe na Baba Lishe wa kisutu watumie nishati ya gesi Taifa kwa matumizi yao mbalimbali .

Aliwataka viongozi wa chama Kisutu na Serikali ya Mtaa huo kuwa walinzi katika majiko hayo ambayo yametolewa Bure soko lote masharti yake gesi ikimalizika ujaze kampuni ya Taifa Gesi .

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu akiwa jimboni anatekeleza Ilani ya chama kwa vitendo .

Mkuu wa Wilaya Ludigija alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza Kampuni ya Gesi ya Taifa gesi wamekuwa WAZALENDO wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanikisha Wananchi watumie nishati ya gesi waachane na kuni na nishati ya mkaa .

Aidha katika hatua nyingine alimpongeza mbunge kutafuta wawekezaji kugawa gesi hizo lengo la Rais wetu zuri, kuwatoa watu Barabarani Wafanyabiashara kuwapeleka maeneo Rasmi Ili waweze kutambulika kwa urahisi limeweza kuzaa matunda Leo wanazawadiwa gesi Bure .

Alisema miti mikubwa iliyokatwa na kusababisha ukame inasababishwa na wakazi wa Dar es Salaam kutumia mkaa hivyo aliwataka Wananchi kutumia Gesi kuacha mkaa inasababisha uhalibifu wa mazingira.

“Taifa gesi ni gesi nzuri inazalishwa nyumbani hivyo Wananchi watumie wamewekeza katika nchi yetu inapatikana nchi nzima alisema Ludigija”

Wakati huo huo Ludigija aliwataka Wafanyabiashara wa mama lishe na Baba Lishe wa Kisutu tukifika mwaka 2024. na Mwaka 2025 wajiandikishe waweze kupiga kura Kumpa ushindi wa kishindo Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Mbunge waJimbo la Ilala Mussa Zungu .

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alipongeza viongozi wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Naibu Spika Kwa Kufanya KAZI kwa vitendo.

Mwenyekiti Sidde alisema nishati ya gesi ni Bora inawaepusha na magonjwa ya mapafu,mkaa unachafua Mazingira wasikate miti ovyo.

Meneja wa Mahusiano wa Taifa Gesi Angel Mwita alisema Taifa Gesi ni kampuni inayosambaza gesi ya Taifa Gesi na Mihani leo tumegawa majiko ya gesi 150 kwa ajili ya kujali Afya kwa Wafanyabiashara wa kisutu Jimbo la Ilala kuunga mkono Juhudi za Mbunge Mussa Zungu .

Angel Mwita alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano alieleza watu watumie Gesi ya Taifa Gesi ni safi na Salama ni gesi yetu bohari kubwa ipo hapa nchini .

Alisema wapo Tayari kushirikiana na serikali kuakikisha Wananchi wanapata huduma Bora ambapo pia aliwataka wanunue vifaa Bora vya Taifa Gesi zikiwemo bana za kampuni hiyo.

Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu zaidi ya shilingi Milioni 7 zimetumika kugawa Majiko ya gesi Ili kuboresha Biashara zao waweze kuwa Katika Biashara za Kimataifa .

Mbunge wa Jimbo la Ilala Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MUSSA ZUNGU leo January 17/2023 amekabidhi majiko ya gesi ya Taifa 150 Bure Kwa Mama lishe na Baba Lishe wa soko la kisutu Ili watumie Nishati ya gesi waache kutumia kuni na mkaa (Picha na Heri Shaaban ).
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija akimkabidhi gesi ya Taifa Gesi Baba Lishe wa soko la Kisutu Leo January 17/2023 yaliotolewa Bure jumla ya majiko 150 katika soko la Kisutu na Mbunge wa Jimbo la Ilala Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu kutoka kwa wadau wake Kampuni ya Taifa Gesi iyopo Dar es Salaam (Picha na Heri Shaaban ).
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde akimkabidhi mtungi wa jiko la gesi Baba Lishe wa soko la Kisutu Jimbo la Ilala majiko hayo yametolewa na Kampuni ya Taifa Gesi Kwa ajili ya Bure Kwa ajili ya Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu Wafanyabiashara wake waache kutumia nishati ya mkaa na kuni na Sasa watumie nishati ya gesi ambayo ni safi na salama kwa matumizi(katikati)Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Taifa Gesi Angel Mwita (Picha na Heri Shaaban ).
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza na Wakazi wa kisutu wakati MBUNGE wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu alipokuwa akikabidhi majiko ya gesi 150 yaliotolewa Kwa ajili ya Mama lishe na Baba lishe wa kisutu majiko yaliotolewa Bure na Taifa Gesi Leo January 17/2023 (kulia )Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde na Mwenyekiti wa CCM kata ya Kisutu Murtaza Darugar (Picha na Heri Shaban ).