December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbowe apokelewa kitengo cha dharura Hospitali ya Aga Khan

Na Penina Malundo, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Chama Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe (Mb), amepokelewa katika Kitengo cha Dharura, Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi wa matibabu zaidi.

Mbowe amehamishiwa katika hospitali hiyo baada ya kushambuliwa usiku wa kuamkia leo na kusababisha kuvunjika mfupa wa nyuma wa mguu na kukimbizwa katika Hospitali ya DCMCT Ntyuka jijini Dodoma.

Mara baada ya kuwasili, Mbowe amepokelewa na jopo la madaktari wa Hospitali hiyo ambao tayari wameshaanza kumfanyia uchunguzi wa jereha hilo.