Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dsm
MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameongoza mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho,Tundu Lissu.
Lissu alikuwa anatarajiwa kuwasili kwenye saa 7:20 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia akitokea Ubelgiji alipokuwa kwa ajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulika jijini Dodoma Septemba 7, mwaka 2017.
Akizungumza na timesmajira online katika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerer Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kisarawe, Alfons Mayugana amesema kurejea kwa Lissu ni matumaini makubwa kwa wama CHADEMA na wapenda Demokrasia nchini.
Amesema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wananchi wanataka kuona mgombea urais anayetokana na uzao wa CHADEMA, hivyo kurejea kwake kunaamsha hilo.
Amesema kuwa mara zote wanaogombea kiti hicho wanatokana na vyama vingine, hivyo kurejea Lissu kunaleta faraja kwa wana CHADEMA kuona safari mgombea anatokana na Chama hicho inatimia.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati