January 21, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbeya City waweka mkakati kulipa kisasi kwa Ruvu

Na Ester Macha, TimesMajira Online, Mbeya

BENCHI la ufundi la timu ya Mbeya City limesema tayari limefashaweka sawa mkakati wao wa kulipa kisasi kwa maafande wa Ruvu Shooting katika mchezo wao wa marudiano namba 256 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) utakaochezwa Mei 13 katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mbeya City itaingia katika mchezo huo huku bado ikiwa inateswa na kipigo cha goli 3-0 walichokipata katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 20, 2020.

Timu hiyo inahitaji alama tatu kwa udi na uvumba ili kujiweka sehemu salama zaidi katika msimam o wa Ligi kwani hadi sasa wapo nafasi ya 13 waliwa na alama 30 walizopata baada ya kucheza mechi 28 na kushinda sita, sare 12 na kupoteza mechi 10.

Lakini pia Mbeya City wanataka kuendelea matokeo mazuri waliyoyapa katika mechi zao zilizopita baada ya kuwafunga Polisi Tanzania goli 1-0, Namungo goli 1-0 na kuibuka na ushindi mnono wa goli 6-1 dhidi ya Maafande wa JKT Tanzania.

Timu hizo zitashuka dimbani huku kila mmoja akihitaji alama tatu kwani hadi sasa katika msimamo wa Ligi timu hizo zote zina alama 27 walizopata baada ya wenyeji kucheza mechi 27 na kushinda tano, sare 12 na kupoteza mechi nne huku JKT wakicheza mechi 26 wakishinda saba, sare sita na kupoteza mechi 13.

Akizungumzia kuelekea katika mchezo huo, kocha mkuu wa timu hiyo, Mathias Lule amesema kuwa, baada ya kufanikiwa kushinda mechi tatu mfululizo, sasa wanahamishia nguvu nyumbani kwao katika mchezo huo dhidi ya Ruvu Shooting.

Almesema kuwa, ushindi katika mchezo huo ni muhimu sana kwao kwani utazidi kuwaweka sehemu salama katika msimamo wa Ligi Kuu ambao sasa hivi wanapambana kujinusuru wasishuke Daraja.

Kocha huyo amesema kuwa, ukiangalia katika ratiba bado wana mechi ambazo ikiwa watafanikiwa na kushinda zote basi watajitoa katika hatari hiyo na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuwapa sapoti.

“tutakuwa nyumbani katika mchezo wetu ujao ambao tutahakikisha hatudondoshi alama yoyote na kwani mkakati wetu ni kuendeleza ushindi ili kuwapa furaha mashabiki wetu hivyo kama timu tupo kwenye maandalizi ili kuhakikisha tunapata ushindi ambao ambao utazidi kutuweka sehemu salama katika msimamo wa Ligi,” amesema kocha huyo.