Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Zanzibar hakuna njaa , wala upungufu wa bidhaa muhimu za vyakula au bei za bidhaa kuwa juu kwenye Masoko kama inavyodaiwa na upinzani.
Kadhalika chama hicho kimetaja shida kubwa iliopo Zanzibar ni upinzani kutaka kutamani madaraka kwa kutumia mbinu batili, uzushi na uongo.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis, alipomaliza kutembelea Soko jipya la Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi Kisiwani Unguja.
Mbeto amesema maisha ya wananchi lwa ujumla yanaendelea kama kawaida, bei za bidhaa ni wastani , Wafanyabishara wanafanya shughuli zao , hakuna aliyepandisha bei kama inavyopotoshwa kwenye mitando ya kijamii .
Amesema njaa ya Zanzibar ni ya kisiasa huku wapinzani wa CCM wakitamani madaraka kwa kutumia hila , uongo na uzushi kwa kudai Zanzibar kuna maisha magumu.
‘Zanzibar kuna njaa ya kisiasa upinzani unalilia madaraka kwa kutumia sera zisizoungwa mkono na wananchi . ACT wanalilia kushika utawala bila kuwavutia wananchi kwa sera makini .Badala yake wanategemea nguvu za uzushi , unafiki na uongo ” Alisema Mbeto
Aidha Katibu huyo Mwenezi, amesisitiza kuwataka viongozi wa ACT ,kuelewe utendajikazi uliofanywa na Serikali ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi kqa miaka minne ,umejenga imani kwa wananchi baada ya kutimiza ahadi zilizoahidiwa kapitia ilani ya uchaguzi na kuleta maendeleo .
“Kila kilichoahidiwa kwenye ilani na ahadi za Rais Dk Mwinyi mwaka 2020 zimetimizwa hatua kwa hatua na kwa wakati sahihi. SMZ haikutaka kuendekeza malumbano ya kisiasa majukwaani badala yake iliweka mkazo kusimamia mabadililo ya kimaendeleo ” Ameeleza
Mbeto amesema takribam Masoko yote yamesheheni bidhaa muhimu kwa ajili ya maisha ya kawaida pia kuna aina zote za vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan zikipatikana .
Hata hivyo Mbeto amewaasa ACT na kuwataka waache siasa za kizushi, zinazokuza mifarakano katika kijamii ilihali wakijua zama hii si zama ya kutegemea udaku, uzushi na uongo kama mtaji wa kisiasa kwa chama makini cha siasa
More Stories
Prof. Kabudi atoa maagizo Saba Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari
Airpay yakabidhi Vishkwambi zitakavyotumiwa na ZEEA katika usajili, uombaji mikopo kidijitali
Tanzania yavunja rekodi,ongezeko la wanyamapori