Na Esther Macha, Timesmajira Online , Mbeya
DEREVA bodaboda mkazi wa Iwambi
Jijini Mbeya ,Juma Afyusisye (38) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa akidaiwa, kumchoma moto mtoto wa jirani yake,ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili,shule ya msingi Iwambi kwa madai ya kutumia fedha aliyomtuma dukani kwa matumizi yake binafsi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga,akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa,Novemba 9,2024,amesema baada ya muathirika kurudi akiwa hana fedha hiyo, ndipo mtuhumiwa alijichukulia sheria mkononi kwa kumwagia petroli kwenye shati alilovaa na kisha kuwasha kiberiti na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
“Mtoto huyu amelazwa hospitali Teule ya Ifisi katika Mji mdogo wa Mbalizi akiendelea kupatiwa matibabu,”amesema Kuzaga .
Aidha Kamanda kuzaga,ametoa rai kwa wazazi na walezi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watafute njia sahihi ya kuwaadhibu watoto pindi wanapokosea.
Kuzaga amesisitiza kuwa jeshi hilo halitavumilia wala kufumbia macho vitendo vya ukatili na unyanyasaji katika jamii.Ambapo litaendelea kuchukua hatua kali kwa watuhumiwa kwa mujibu wa sheria.
More Stories
Waziri Lukuvi aeleza maono ya Isimani ijayo
Madiwani Korogwe TC wahakikishiwa maji ya uhakika
CHADEMA wampongeza Mkurugenzi Mpanda