-Ni baada ya kuwapasua mafuvu ya vichwa hadi kumwaga ubongo.
Na Moses Ng’wat, TimesMajira Online, Songwe.
POLISI mkoani Songwe limemkamata, Aloyce Nyabwanzo (51), Mkazi wa kitongoji cha Kikamba, kijiji cha Kapalala Wilayani, Songwe kwa tuhuma za kuwaua wajukuu zake wawili kwa kuwapasua mafuvu ya kichwa na mchi wa kutwangia mahindi hadi ubongo kumwagika.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya, amesema tukio hilo lilitokea Aprili 30,2023 majira ya saa 5:00 usiku na kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kujua sababu za mtuhumiwa kutenda tukio hilo.
Amesema mtuhumiwa alitumia mbinu ya kuwavizia wajukuu zake hao wakati wanatoka chumbani kwao kumfuata bibi yao sebuleni aliyekuwa anajaribu kuzuia mlango usivunjwe na mtuhumiwa huyo baada ya kuanzisha vurugu nyakati hizo za usiku.
“Marehemu wamefanyiwa uchunguzi na daktari na kubaini kuwa vifo vyao vimesababishwa kupasuka kwa mafuvu ya kichwa baada ya kupigwa na kitu kizito hali iliyosababisha kuvuja damu nyingi na ubongo kutoka nje” amesema Kamanda Mallya.
“Marehemu wamefanyiwa uchunguzi na daktari na kubaini kuwa vifo vyao vimesababishwa kupasuka kwa mafuvu ya kichwa baada ya kupigwa na kitu kizito hali iliyosababisha kuvuja damu nyingi na ubongo kutoka nje” alisema Kamanda Mallya.
Amewataja marehemu hao waliouawa kwa kupasuliwa mafuvu ya kichwa kuwa ni Jackson Chacha (2) na George Chacha (5) wote wakazi wa kitongoji cha Iwindu- Kikamba katika kijiji cha Kapalala na walikuwa wakilelewa na mtuhumiwa.
Hata hivyo, Kamanda Mallya amesema wakati uchunguzi wa kujua sababu zilizosababisha mtuhumiwa kutenda tukio hilo, mtuhumiwa atapelekwa hospitali ili kupimwa afya ya akili.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba