Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
WAZIRI wa Maji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Profesa Makame Mbarawa amechukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar.
Profesa Mbarawa amechukua fomu leo asubuhi katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui, ambako alikabidhiwa fomu na Katibu wa Oganaizesheni wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Galous Nyimbo.
Profesa Mbarawa ambaye pia amehudumu uwaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, anakuwa mwanachama wa 10 wa CCM kuchukua fomu tangu zoezi lilipoanza Jumatatu wiki hii


More Stories
Watendaji ,viongozi wapewa elimu ya udhibiti
Chawino kufanya uchaguzi mdogo
NBS yasisitiza matumizi sahihi ya Takwimu katika Madini