December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbaga wa Ilala aunga mkono kampeni ya Usafi

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Diwani Mstaafu wa Upanga Magharibi Godwini Mbaga, ameunga Mkono kampeni ya Usafi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya Pendezesha Mji wa Dar es Salaam kwa kuchangia shilingi milioni 1 ya vifaa vya USAFI Ili Ilala iwe safi.

Akizungumza na waandishi wa habari Godwini Mbaga, amesema amepongeza Mkuu wa Mkoa Amos Makala, kwa kampeni yake endelevu ya usafi ambayo inaendelea hivyo lazima wadau tumuunge mkono mji unavyokuwa msafi Ikiwemo Wilaya ya Ilala .

” Tunashirikiana na Mkuu wa Mkoa Katika kuweka Mji katika usafi ni jambo la kuigwa Wafanyabiashara wanasafisha mji kwa kucheza Mziki suala la usafi la mtu mwenyewe kuakikisha Mazingira yanakuwa safi ” amesema Mbaga .

Aidha Mbaga amepongeza Profesa Mohamed Janab wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuonyesha kwa vitendo kampeni ya usafi ametoka hospitali anajumuika na Wananchi ni jambo jema ambapo amezungumza mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anapanga mikakati ya kuwatafutia Wafanyabiashara eneo Maalum ambalo watakuwa wanauza bidhaa zao yakiwemo matunda kwa ajili ya wagonjwa .

Ametoa Rai kwa Wananchi wote wa Upanga Mangaribi na Wilaya ya Ilala waunge mkono juhudi za Usafi endelevu ambazo zinafanywa na Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Amos Makala, na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch,Ng’ wilabuzu Ludigija.Aliwataka Wananchi wa Wilaya ya Ilala kutupa na kuifadhia taka Katika vifaa Maalum ikiwemo Dastbini .

Awali Mkuu wa mkoa alimpongeza Diwani Mstaafu wa Upanga Mangaribi Godwini Mbaga ambaye ametoa ahadi ya kukabidhi shilingi milioni 1 Katika kampeni hiyo na Mkuu wa Mkoa Amos Makala alimuomba akamkabidhi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dar Es Salaam atampa lisiti .

Kampeni ya Usafi Octoba 29 mwaka huu zilifanyika Upanga Magharibi nje ya eneo la hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na BARABARA za eneo hilo .