Na Mwandishi Wetu, TimesMajira OnlineĀ
NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amesema hivi sasa magonjwa yasiyoambukiza ndiyo yanaendekezwa katika jamii kwani watu wamekuwa wanakula hovyo, kuvuta sigara na kunywa pombe.
Zungu amesema hayo hivi karibuni, Dar es Salaam baada ya kuzindua kampeni ya ‘Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo wako’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupambanana magonjwa hayo.
Uzinduzi huo uliyoambatana na zoezi la matembezi, Zungu amesema magonjwa yasiyoambukiza ndiyo jamii inayakimbilia na kuyaona ndiyo matamu zaidi.
“Na magonjwa haya matamu tunayoyakimbilia yameongezeka kwa asilimia 40 kwa vijana kwa sababu tunakula hovyo, tunavuta sigara na tunakunywa pombe hovyo, kinachotakiwa ni kufanya mazoezi,” amesema Zungu
Pia, amesema takwimu zinaonesha vijana wanaongoza kwa maambukizi ya ukimwi kwa asilimia 40, ambapo ni hatari sana, wajaribu kuepuka kufanya ngono ambayo siyo salama.
“Zoezi hili tutaendelea nalo, makundi yote yaĀ jogging tutayaleta hapa yana watu sio chini ya 5,000 watakuja kushiriki katika matembezi na mapambano ya kupinga magonjwa ya kuambukiza,”amesemaĀ
Leo tumezindua zoezi hili lakini litapamba moto mwishoni mwa Desemba au Januari mwakani ambapo makundi mengi yatajiunga ili na wao waweze Kupambana na maradhi ambayo hayaambukizi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt Peter Kisenge amesema magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo yamekuwa ni magonjwa yanayosababisha vifo vya watu wengi duniani.
Amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa watu milioni 17.3 duniani kote ikiwemo Tanzania wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo.
Pia, amesema utafiti wa kitaifa wa STEP uliyofanyika nchini Tanzania mwaka 2012 kuhusu mambo hatarishi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ulionesha kuwa kati ya watu wazima asilimia 15.9 walikuwa wanatumia tumbaku au sigara.
“Asilimia 26 walikuwa na viwango vya juu vya lehemu yaani mafuta yaliyozidi mwilini na asilimia 97.2 walikuwa hawatumii mboga mboga angalau siku tano kwa wiki, chini ya asilimi tano walikuwa wakila matunda angalau siku tano kwa wiki,”amesema Dkt Kisenge
Dkt Kisenge amesema asilimia 29.3 katika utafiti huonwaliku wakinywa pombe na asilimia 26 walikuwa na uzito uliozidi. Kiwango cha maambukizi ya kisukari kilikuwa ni asilimia 9.1 na shinikizo la damu kilikuwa ni asilimia 25.9.
“Tumezindua matembezi ya kilomita tano kwa ajili ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa ya moyo ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi duniani,” amesema.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu