Na Penina Malundo
MAWAZIRI kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wamekutana nchini Tanzania kujadili na kuangazia hali ya usalama ya nchini Congo inavyoendelea kwa hivi sasa.
Miongoni mwa Mawaziri na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wameweza kuhudhulia kikao hicho jijini Dar es Salaam ikiwemo nchi ya Angola,Malawi,Afrika ya Kusini ,Zambia ,Zimbabwe, DRC-Bostwana,Tanzania, Uganda,Sudan ,Somalia ,Rwanda,Kenya na Burundi.
Akizungumza katika ufunguaji wa mkutano huo,Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri hao kutoka SADC, Profesa Amon Murwira amesema kikao hicho cha mawaziri kimeitishwa muda mfupi kutokana na hali tete ya DRC Congo inavyoendelea.
Amesema uwepo wa mawaziri hao katika kikao hicho ni uimarishaji wa ulinzi na usalama sio tu kwa nchi ya Congo bali kwa nchi zao zote.
“Tukio hili ni la kihistoria hivyo kupitia mchakato huu utafute amani ya kudumu kwa Mapigano yanayoendelea katika mji wa Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwani kupoteza kwa Wanajeshi 16 na Raia 700 huku raia wengine laki nne waliohama goma kwa mwaka huu.
“Waasisi wetu walianzisha SADC kwa malengo yake na kuhakikisha dira ya Sadc inafatwa ikiwemo ya kuungana nakufanya kazi kwa pamoja ili kulinda rasirimali na kuwezesha wananchi kujitegemea kwa kuisha maisha yaliyobora,”amesema.
Amesema hali ya Kiusalama na hali za binadamu nchini Congo bado ipo tete licha ya juhudi ya Rwanda ja Nairobi kufanya mazungumzo kupitia Rais wa zamani Kenyata.
“Hali hii inatufanya kusimama imara kuhakikisha suluhu inapatikana kwani hatujawahi kuona suluhu yoyote inapatikana kwa mitutu zaidi ya kukaa chini na kufanya mazungumzo.
“Wote tunakumbuka amani na usalama ni muhimili wa msingi katika bara letu na ukuaji wa kiuchumi hivyo inabidi tutumie hali ya Kidiplomasia na kisiasa kuhakikisha hali hii itulie.
“Wakati tukijadili hapa tukiendeleza migogoro hii na kulipiza visasi tutakuwa vipofu hivyo naamini kikao hiki tutatoka na suluhisho muhimu la pamoja ambalo tutaliwasilisha kwa wakuu wa nchi zetu,”amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Ujumbe wa Mawaziri wa EAC, Musalia Mudavadi amesema mkutano huu ni matokeo ya jumuiya zao zote mbili kukubaliana kwa pamoja katika kujadili hali ya usalama ya nchini Congo.
“Lazma tuchukue maamuzi ya kurudisha hali ya amani na haki za binadamu kwa wananchi wa Congo,mgogoro ubagharimu mambo mengi ikiwemo njaa,ukame hata hali ya kiuchumi hasa kwa wanawake na watoto.
“Kadri mgogoro unavyoendelea utasababisha rasilimali na chumi zetu kufanya vibaya,Mkutano huu utatoka na maazimio ya pamoja kutoa muongozo wa njia ya kuifata kwani kuna umuhimu wa kutoa wito wa kusimamisha vita haraka sana na kufanya mazungumzo ya pamoja,”amesema.
Aidha amesema ni vema kuhakikisha haki za binadamu zinapatikana na kuheshimua sheria za kimataifa na za kidplomasia.”Tunatoa wito kusitishwa kwa mapigano haya na wahusika wazungumze njia ya kupata suluhu kwani mapigano yanayoendelea sio njia ya suluhu,”amesisitiza.
Amesema licha ya kuwepo kwa mazungumzo mengi,majawabu ya mgogoro huu yanapaswa kutoka kupitia mkutano huo na kutoka na maazimio ya pamoja yakutoa matokeo ya mchakato mzima.
More Stories
Maadhimisho siku ya Kimataifa ya Wanawake na wasichana katika sayansi kufanyika Dodoma
Watanzania wakumbushwa kudumisha na kulinda amani
Mbaruku:Lushoto haikutakiwa kuwa na shida ya maji