May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mawakala zaidi 200,000 wakumbushwa wajibu wao

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

KAMPUNI ya simu ya Tigo Tanzania imeendelea kuboresha huduma zakeĀ  kwa kukaa pamoja na mawakala na kuwakumbusha jinsi ya kuhakikisha wanafanya miamala sahihi kwa wateja wao nchi nzima.

Hayo yalisemwa juzi na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelika Pesha, wakati alipokutana na wamawakala zaidi ya 200,000 kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kusheherekea mafanikio waliyoyapata mwaka 2023 na kueleza mikakati ya kuboresha huduma zao kwa mwaka 2024.

“Lengo la mkutano huu ni kutoa elimu kwa mawakala kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika kazi zao ikiwemo matapeli wa mitandaoni, ambapo mawakala wetu wanatakiwa kuhakikisha wanafanya miamala sahihi kwa mteja sahihi,” alisema na kuongeza;

“Sisi kama tigopesa tuna mawakala zaidi ya 200,000 ambao wanapatikana nchi nzima na tumegawanyika katika zone mbalimbali ikiwemo Zanzibar, North, South, Pwani, hivyo leo tuna mawakala kutoka nchi nzima,” alisema Pesha

Kwa upande wake, Gladness Kazimoto,  Wakala wa Tigo mkoani Dodoma aliiomba Serikali kuendelea kutoa elimu kwa mawakala ili kuepukana na wizi wa mitandaoni

“Kipindi cha nyuma mawakala walikuwa wanaibiwa sana tofauti na sasa, hivyo tunaendelea kuipongeza Serikali na tunashukuru kwa jinsi ambavyo na wenyewe wameendelea kutoa elimu kwa mawakala wetu ambao ni wadogo wadogo “

NayeĀ  Wakala Mkuu wa Tigopesa kwa Mikoa yaĀ  Mbeya na Ruvuma, SaidĀ  Mdee, alisema katika shughuli za wakala mkuu wameweza kufanya shughuli mbalimbali, ambapo Tigo wamewainua kwa namna mbalimbali ikiwemo kuweza kupata faida nyingi za kifedha.

Wakala kutoka Tanga, Kilimanjaro na Arusha, AbdulAziz Lema alisema utofauti walipotoka na sasa walipo ni mkubwa, hivyo aliwashukuru Tigo kwa kuweza kuwapa ajira kwao wenyewe na kwa Watanzania wengine ikiwemo vijana.