Na Pendo Mtibuche, TimesMajira Online, Dodoma
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Antony Mavunde amesema atahakikisha anarinda heshima ya chama kilichompitisha kukiwakilisha na kufanya kampeni za kistarabu katika jimbo lake na siyo matusi na kejeli.
Akizungumza hayo mara baada ya kuchukua fomu za uteuzi wa mgombea ubunge katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi alisema kuwa hana mpango wa kufanya kampeni za kejeli wala matusi kwani wananchi wanataka maendeleo.
Alisema kuwa anakishukuru chama kilichomuamini na kumpitisha kupeperusha bendera yake hivyo jambo la msingi ni kuwa wastarabu na kulinda heshima ya chama.
Alisema kuwa wanachama wanachotaka ni maendeleo na siyo kufanya kampeni za kutukanana, kudhalilishana jambo ambalo alisema kuwa yeye anataka kuwa wa mfanao katika kampeni hizo.
Kwa upande wake naye msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini Msekeni Mkufya akimkabidhi fomu mgombea hiyo alisema kuwa yapo mambo ya msingi ambayo muhusika anatakiwa kuyafuata ili kuweza kukamilisha fomu hiyo ya uteuzi wa mgombea ubunge.
Alisema ndani ya fomu hiyo kuna vitu mbalimbali vya kuzingatia ikiwemo muhusika ahakikisha anakuwa na wadhamini wasiopungua 25 hadi 31 na wadhamini hao wasiwe wamemdhamini mtu mwingine.
Mambo mengine ya kuzingatia ni pamoja na fomu hiyo ilipiwe kiasi cha sh.50,000 lakini pia alikabidhiwa kanuni mbalimbali ambazo zitamwezesha kuzifuata pindi anapotekeleza majukumu yake.
Hata hivyo msimamizi huyo wa uchaguzi alisema kuwa tika Jimbo la Dodomaml Mjini lina vituo 911 vya kupigia kura hivyo mgombea anatakiwa kuwa na mawakala watatu katika kila kituo jambo ambalo alisisitia kuwa mgombea anatakiwa kuwa na mawakala waelewa.
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani